top of page
Mchomokinga
Mwandishi:
ULY CLINIC
14 Juni 2021 18:02:56
Michomokinga ni nini?
Ni tendo asili la mwitikio wa mwili kwenye vichokoza mwili vya hatari kama vile bakteria, virusi, chembe zenye jeraha au vikereketa mwili.
Ni njia ya mfumo wa kinga kupambana na maradhi kwa kuzalisha antibodi na chembe nyeupe za damu ili kushambulia maambukizi au majeraha yaliyotokea.
Eneo lililo na maambukizi au majeraha linapotembelewa na kemikali, antibodi na chembe nyeupe za damu huwa na dalili za ujoto, wekundu, uvimbe, maumivu na kupoteza uwezo wa kufanya kazi. Kwa jina jingine hufahamika kama 'inflammation'.
Imeboreshwa,
21 Septemba 2024 12:55:57
bottom of page