top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Anafailaksia

Anafailaksia

Ni mzio mkubwa wa dawa unaotokea dakika chache tu baada ya kutumia dawa au kitu kinachosababisha mzio.

Anajizia

Anajizia

Ni upotevu wa hisia kwenye maumivu, ni ishara muhimu ya ugonjwa katika mfumo wa kati wa fahamu, na mara nyingi hutoa ishara ya sehemu gani haswa ya uti wa mgongo ina shida.

Antibodi

Antibodi

Antibodi ni ni protini zinazozalishwa kwenye damu kuitikia uwepo wa antijeni kwenye damu.

Antijen

Antijeni

Ni protini yenye uwezo wa kuamsha mfumo wa kinga ya mwili kuzalisha antibodi.

Azuma

Azuma

Azuma au AZUMA ni jina la kibiashara la Azithromycin ambayo ni dawa jamii ya antibayotiki iliyo kwenye kundi la macrolide, hutumika kutibu maradhi mbalimbali ikiwa yenyewe au na mchanganyiko wa dawa zingine.

bottom of page