top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Kichefuchefu baada ya kula

 

Kichefuchefu cha kawaida kinaweza kusababishwa na hali au vitu mbalimbali vinavyoendelea ndani ya mwili. Vivyo hivyo kichefuchefu baada ya kula pia huweza kuchangiwa na hali au vitu mbalimbali vinavyoendelea ndani ya mwili na huweza ambatana na dalili zingine ambazo huelezea ni nini kisababishi.

 

Makala hii imejikita kuzungumzia kuhusu  visababishi, ugunduzi, matibabu na kinga.

 

Visababishi

 

Vipo visababishi vingi vya kichefuchefu baada ya kula ambavyo vimeorodheshwa hapa chini, bonyeza aina ya kisababishi kusoma zaidi kuhusu dalili zingine ambazo huambatana;

 

 

Namna gani visababishi hugunduliwa?

 

Visababishi hugunduliwa kutokana na historia ya tatizo kwa mgonjwa, daktari atakuuliza maswali mbalimbali kujua shida yako kabla ya kuamua kufanya vipimo. Utaulizwa maswali kulingana na nini amefikilia kuwa ni sababu kutoka kwenye dalili zingine ambazo utakuwa umezitaja. Kwa jinsia ya kike utaulizwa kuhusu ni lini mara ya mwisho umeona siku zako, na kama una ujauzito. Vipimo ambavyo daktari anaweza agiza kufanyika kuligana na alichofikiria kuwa ni kisababishi kwako ni;

​

  • Kipimo cha aleji kwenye ngozi

  • Kipimo cha CT

  • Kipimo cha damu

  • KIpimo cha kamera kuangalia koo na mrija wa esofagasi

  • Kipimo cha kolonoskopi au sigimoidoskopi

  • Kipimo cha mkojo

  • Kipimo cha Ultrosound

  • Kipimo chaX ray

 

Matibabu

 

Matibabu mara nyingi hutegemea na kisababishi ambacho kimeonekana,

​

  • Endapo unatumia dawa aina Fulani zinazosababisha kichefuchefu utashauriwa upunguze kiasi cha chakula unachokula au kutumia dawa za kuzuia kichefuchefu

  • Kwa wagonjwa wenye tatizo la Kucheua tindikali, utashauriwa kuzuia kula vyakula vyenye viungo kwa wingi, mafuta kwa wingi na kupunguza uzito. Pamoja na hivyo utapewa dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali tumboni.Soma zaidi kuhusu kucheua tidikali kwa kubonyeza hapa

  • Kwa wagonjwa wenye homa ya mwendo, unashauriwa unapokuwa safirini ukae sehemu ambayo hutaona mwendo wa chombo cha kusafiria ili hali yako isiamke

  • Kwa wagonjwa wenye kichefuchefu kutokana na magonjwa ya kibofu cha nyongo mfano mawe au maambukizi, maambukizi hayo yatatibiwa kwa dawa za kuyeyusha  au kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mawe

  • Kwa  wajawazito, utashauriwa kuhusu matumizi ya chakula ambacho hakileti kichefuchefu, endapo hali inaambatana na kutapika basi utapewa dawa za kuzuia kichefuchefu. Soma zaidi kuhusu kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito kwa kubonyeza hapa.

  • Kwa wale ambao kichefuchefu kimesababishwa na mzio wa chakula, utashauriwa kuacha kutumia vyakula ambavyo vinaleta mzio kwako endapo kisababishi ni mzio wa chakula

  • Wagonjwa wenye msongo wa mawazo na ang’zayati, daktari atakushauri kuhusu mazoezi ya yoga na namna ya kukabiliana na tatizo hili

  • Wagonjwa wenye sindromu ya iritabo, utashauriwa kuachana na vyakula ambayo vinaamsha tatizo lako na matumizi ya dawa

 

Soma kuhusu dawa za kuzuia kichefuchefu kwa kubonyeza hapa.

​

Kinga

 

Unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kujikinga au kupunguza hali ya kicehfuchefu,

 

  • Nyonya au lamba vipande vya barafu, unaweza kutia mdomoni vipande vidogo ili kuvinyonya vema

  • Acha kutumia vyakula vyenye mafuta, vilivyokaangwa au vyenye viungo vingi

  • Kula vyakula vikavu na asilia kama bisi, n.k

  • Kula chakula mara kwa mara badala ya kula mlo mmoja mkubwa

  • Tulia chini baada ya kula, usitembee au kuamka ghafla mara baada ya kula chakula

  • Kula taratibu na unapokunywa maji pia, kunywa taratibu

  • Endapo harufu ya chakula kilichopikwa kinakufanya upate kichefuchefu, kula chakula wakati kimepoa

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako endapo umeona kuwa na shida yoyote ile baada ya kusoma makala hii kabla ya kujichukulia hatua binafsi.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au bonyeza "Pata Tiba" chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshwa, 28.12.2020

​

Rejea za mada hii,

​

bottom of page