top of page

Kichocho

​

Imeandikwa  na daktari wa uly clinic

​

Kichocho, ugonjwa unaofahamika kwa lugha ya tiba schistosomiasisi, ni ugonjwa unaofahamika kwa jina jingine la bilharzia. Ugonjwa huu husababishwa na minyoo na unaweza kuwa wa muda mfupi au au ugonjwa sugu.

 

Ugonjwa huu ni wa pili  kuathili au kuwapata watu katika bara la Afrika ikiongozwa na malaria. Ugonjwa wa kichoho umeonekana kutotiliwa umaanani katika ukanda huu wa jato.

​

Kimelea anayesababisha kichocho huishi kwenye maji yasiyo na chumvi na huishi ndani ya konokono. Kimelea anayesababisha kichocho anatengenezwa ndani ya konokono hufahamika kwa jina la serkaria huishi kwenye maji baada ya kutoka kwenye konokono,.

 

Mtu akiwa anaogelea haswa mida ya sa sita mchana, vimelea hawa hupenya kwenye ngozi ya mtu huyu  na kuingia katika mfumo wa damu. Maambukizi mengi ya kichocho hutokana na vimelea wanaoitwa Schistosoma (S) Mansoni, S.Hematobium na S.Japonicum 

 

Maambukizi yanatokeaje

 

Maambukizi  hutokea endapo mtu ataogelea kwenye maji yenye konokono wanaobeba vimelea vya kichocho, na endapo mtu aliyeambukizwa atajisaidia haja kubwa au ndogo kwenye maji hayo. Vimelea wanaowekwa na mtu aliyeambukizwa kwenye madimbwi ya maji husambaa kwenye maji hayo na  kuendeleza mzunguko wa maambukizi kwa watu wengine.

 

Mara baada ya mtu kumwaga mayai katika maji(wakati wa kujisaidia haja kubwa au ndogo), haya huingia kwa konokono na baadae hutotolewa na kuzalisha minyoo inayoitwa serkaria. Minyoo hii  hutoka nnje ya konokono na kuingia kwenye mwili wa binadamu kupitia ngozi.

 

Sekaria huweza kuishi mpaka masaa 48 baada ya kutoka ndani ya konokono na baadae hufa, mtu anaweza kupata maambukizi ya vimelea hawa endapo atakuwa anafua, kuoga, kuogelea au kuosha vyombo kwa maji yenye maambukizi ya vimelea hivyo.

 

Mara baada ya kuambukizwa, vimelea hukaa katika mishipa ya damu ili kukua na baada ya kukua hukutana kimwili na vimelea vya kike na kisha kutaga mayai. Mayai haya husafili kuelekea kwenye kibofu cha mkojo au matumbo/utumbo na kisha kutolewa kwa njia ya mkojo au kinyesi.

​

​

Endelea kusoma makala hii kwa kutumia email yako

​

Bonyeza kusoma kuhusu DaliliDalili za maambukizi sugu ya kichochoUchunguzi & matibabu

​

ULY clinic inakukumbusha uwasiliane na daktari wako endapo umaona kuwa una dalili zozote zilizotajwa katika makala haya.

​

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa Elimu, ushauri na Tiba kwa kubonyeza hapa au bonyeza neno Pata Tiba chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshw mara ya mwisho 21.04.2020

​

Rejea za mada hii

​

1.Schistosomiasis.WHO.https://www.who.int/newsroom/factsheets/detail/schistosomiasis. Imechukuliwa 20.04.2020

​

2.Schistosomiasis.CDC. https://www.cdc.gov/parasites/schistosomiasis/index.html. Imechukuliwa 20.04.2020

​

3.Schistosomiasis(Bilhazia).NHS. https://www.nhs.uk/conditions/schistosomiasis/. Imechukuliwa 20.04.2020

bottom of page