KICHWA MAJI (Haidrosefalazi)
Imeandikwa na daktari wa uly clinic
Haidrosefalazi kwa lugha ya kiswahili kichwa maji, ni tatizo linalotokana na kuharibika kwa mfumo wa uzalishaji, ufyonzaji na usafilishaji wa maji yaliyo kwenye mfumo wa fahamu yanayoitwa Maji ya serebro spaino-CSF.
Kwa kawaida maji haya yaliyo katikati ya vyumba vya ubongo na Uti wa mgongo huwa na kazi ya kuulinda ubongo na uti wa mgongo dhidi ya mitikisiko, kuupatia chakula na kuhusika kuondoa sumu za kimetaboli.
Uzalishaji wa maji haya huenenda sawa sawa na ufyonzwaji, maji huzalishwa sehemu moja na kufyonzwa sehemu nyingine ndani ya ubongo na hivo husafili kwenye njia na milango mbalimbali.
Endapo kuna tatizo lolote linalofunga/kuziba milango au linalozuia ufyonzaji au kuongeza uzalishaji wa maji, maji haya huwa mengi na kusababisha kutanuka kwa vyumba vinavyopitisha maji na kusababisa ujazo na ukubwa wa kichwa kuongezeka sana kwa watoto. Dalili za watu wazima huwa tofauti na watoto.
Kwa kawaida kuna usawia wa viungo na maji yaliyomo ndani ya kichwa, usawia huu hupelekea kutobadilika kwa shinikizo la ndani ya vyumba vya ubongo. Endapo kitu chochote kikiongezeka ndnai ya ubongo, kinaweza kusababisha shinikizo kuongezeka na kuleta madhara kweney mfumo wa fahamu.
Maji yanapoongezeka ndani ya vyumba hivi husababisha kusukuma kuta za ndani ya ubongo kutanua vyumba na kugandamiza au kuharibu ubongo kabisa. Kwa watoto wadogo kwa vile fuvula kichwa huwa halijaungana huonyesha dalili ya kuwa na kichwa kikubwa pamoja na dalili zingine.
Maji yanapoongezeka ndani ya kichwa na kwa sababu mifupa ya watu wazima haiwezi kutanuka basi husabisha kuongezeka kwa shinikizo la ndani ya kichwa tu pamoja na madhara yatokanayo na kugandamizwa kwa ubongo
Tatizo la haidrosefalas lisipotibiwa mapema linaweza kusababisha makubwa na hata kifo kwa mfano ubongo ukiwa unasukumwa kutokana na kuongezeka kwa shinikizo ndani ya ubongo husababisha tishu za ubongo kupenyeza kwenye maeneo ya matundu ya kichwa. Sehemu zinazopenyeza hufa kutokana na mgandamizo, ubongo katika sehemu zilizogandamizwa Hushindwa kufanya kazi yake vema ikiwa pamoja na sehemu zinazoongoza mfumo wa upumuaji. Kusimama kwa mfumo wa upumuaji hupelekea kifo.
Wazee nao huweza kupata tatizo hili lakini kwa sababu mtu anapozeeka ujazo wa ubongo hupungua, kuongezeka kwa maji hakusababishi matatizo ya kuongezeka shinikizo la ndani ya kichwa linaloitwa hydrosefalazi ya yenye shinikizo la kawaida-NPH. NPH huchangia asilimia 40 tu ya ugonjwa wa hydrosefalazi na ile inayotokea kwa watoto huwa na asilimia 60
Tatizo hili halibagui jinsia, hutokea sawa sawa kwa wanaume/wanawake na watoto bila ubaguzi. Umri wa kutokea tatizo hili mara nyingi huwa utotoni, matatizo makubwa huonekana ukubwani kama mtoto hajapata matibabu mapema.
Nini husababisha kichwa maji(Haidrosefalazi)?
Bonyeza hapa kuendelea kusoma. Itakuhitaji uwe na barua pepea tu
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua inayodhuri afya yako.
Wasiliana na daktari wa ULY clinci kwa kuuliza mwswali ushauri na matibabu kwa kubonyeza hapa
Rejea za mada
Rejea
1. NIH. Hydrocephalus. https://www.nhs.uk/conditions/hydrocephalus/. Imechukuliwa 18.04.2020
2. Mediscape. Hydrocephalus. https://emedicine.medscape.com/article/1135286-overview. Imechukuliwa 18.04.2020
3. Healthline. Hydrocephalus. https://www.healthline.com/health/hydrocephalus. Imechukuliwa 18.04.2020
4. Hydrocephalus association. Hydrocephalus. https://www.hydroassoc.org/what-is-hydrocephalus-an-overview/. Imechukuliwa 18.04.2020
5. Medical news today. Hydrocephalus. https://www.medicalnewstoday.com/articles/181727. Imechukuliwa 18.04.2020