Imeandikwa na Daktari wa ULY-clinic
​
​
Maumivu ya kifua
​
Visababishi vya maumivu ya kifua vinaweza kuwa pamoja na;
​
Infaksheni ya mayokadia
Husababisha maumivu ya kifua ya kuchana nyuma ya stenamu, yanayoelekea upande wa kushoto wa bega. Huwa hayaponi kwa matumizi ya dawa jamii ya glyceryl trinitrate. Maumivu haya huweza kusababisha kichefuchefu na kutapika.
​
Anjaina ya Pektoris
Husababisha maumivu ambayo yanaweza kusambaa bega na mkono wa kushoto. Mtu huwa na historia ya maumivu haya. Hupona ndani ya dakika tatu za kutumia dawa za glyceryl trinitrate.
​
Maumivu ya tumbo ya ghafla
Sehemu maumivu yalipo katika tumbo ni jambo la muhimu kufahamu. Maumivu haya yanaweza kusababishwa na ugonjwa wa kucheua tindikali(GERD), kichefuchefu, kutapika, kuharisha, haja ngumu, manjano, melena, hemachuria, hematemesis, kupoteza uzito, na mrenda au damu kwenye kinyesi.
​
Anurizimu ya kupasua
Husababisha maumivu ya ghafla ya kifua au nyuma ya mgongo,maumivu huwa kama ya kuchana, kusaga yanayosambaa chini ya mgongo na kuambatana na kupoteza fahamu na kuishiwa pumzi.
​
Esofajaitis
Maumivu huhisiwa nyuma ya mfupa wa stenamu mtu akilala au kupinda kuelekea mbele. Maumivu huwa nafuu mtu akitumia dawa jamii ya antasidi
​
Mgonjwa mwenye shauku kali huweza kuwa na maumivu kwenye maeneo moyo ulipo, hupumua kwa haraka Zaidi, huwa amepaniki na kupata maumivu kwenye maeneo ya moyo.
​
Majeraha
Mtu atakuwana historia ya jeraha kwenye kifua
Maambukizi kwenye kifua au uvimbe
-
Maumivu hutokea wakati wa kuvuta hewa au kukohoa
-
Huweza kuambatana na disipnia na kikohozi
​
Embolizimu ya palmonari
Hutokea pale endapo damu iliyoganda ikiweka makazi wkenye mshipa wa arteri wa pulmonari, na kuzuia damu kutembea sehemu zingine za mapafu.
​
Kubomoka kwa mapafu
Maumivu haya huanza ghafla na hudumu kwa madaa kadhaa, huambatana na kuishiwa pumzi. Mapafu kubomoka hutokea endapo hewa imeingia kati ya mapafu na mbavu.
​
Mkanda wa jeshi
Husababishwa na kuamshwa kwa tetekuwanga, huambatana na na maumivu ya kifua pamoja na mkanda wa malenge lenge nyuma ya mgongo au kifuani
​
Endelea kusoma kuhusu maumivu ya kifua yanayohusiana na moyo
​
pia
​
Bonyeza kusoma makala zingine kuhusu; maumivu ya katikati ya kifua​, kifua kubana na kuwaka moto
​
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba
​
​
​
Imeboreshwa 05.08.2020
​