Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
Kiharusi-Stroke
Kiharusi/stroke ni tatizo linalotishia maisha, hunasababishwa na kunyimwa au kupungua kwa damu katika sehemu yoyote ya ubongo. Mtu akipata kiharusi anatakiwa apate matibabu ya haraka ili kuweza kupunguza madhara makubwa yanayoweza kuendelea katika ubongo, matibabu yakifanyika mapema madhara yanakuwa madogo.
Kwanini kiharusi kinatokea?
Kama ilivyo ogani mbalimbali mwilini zinavyohitaji sukari kwa ajili ya kuzalisha nishati, Ubongo nao unahitaji virutubisho na sukari kufanya kazi zake, endapo vikipungua kwa kiasi kikubwa chembe hai za ubongo hufa na kusababisha tatizo kwenye ubongo na ulemavu au kifo. Kunyimwa kwa damu ama kupungua kwa damu inayoenda sehemu fulani ya ubongo husababisha ubongo kukosa sukari na virutubisho, na hili kuleta chembe za ubongo hufa ndani ya dakika chache, endapo damu itaelekea katika maeneo hayo basi ufanyaji kazi wa ubongo unaweza huishwa tena.
Kuna sababu mbili zinazoweza kusababisha kiharusi
-
Mishipa ya damu kuziba na kusababisha damu kutofikia chembe hai za ubongo , Huchangia kwa asilimia 85 ya Viharusi vyote
-
Kuvilia kwa damu.Hutokana na kupasuka au kuchanika kwa mishipa ya damu iliyo ndani ya ubongo.Hili huusababisha damu isifike kule iendako
Kuna kiharusi kingine kinachoitwa "kiharusi cha mpito" (TIA) ambapo mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo inaziba kwa kipindi cha mpito na kuachia . Dalili za kiharusi hiki hukaa kwa muda wa dakika 30 hadi masaa kadhaa na kupotea. TIA hutakiwa kutibiwa kwa matibabu ya uharaka na uhakika maana siku zote huleta ishara kwamba kuna kiharusi kinaweza kutokea hapo mbeleni kidogo ambacho huweza kusababisha madhara makubwa ama kifo.
Dalili za tatizo la kiharusi ni zipi? Bonyeza hapa kuendelea kusoma