Kisukari
​
Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
​
Kisukari (Diabetes mellitus) ni kundi la magonjwa linalotokana na kuathirika kwa mfumo wa utumiaji sukari mwilini. Sukari ni chanzo cha nguvu mwilini mara inapoingia katika chembe hai, hivyo ina umuhimu kwa kuendeleza maisha ya chembe hizi. Ubongo hupata nguvu za kuweza kufanya kazi kwa asilimia kubwa kutoka kwenye sukari(glucose) na isipokuwepo inaweza kuleta madhara kama kuzimia n.k
Mtu akiwa na kisukari pasipo kutegemei aina gani, kinachotokea ni kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika mzunguko wa damu na hivyo huleta matatizo makubwa kwenye ogani mbalimbali mwilini.
Matatizo sugu ya kisukari yanaweza kugawanyika katika sehemu mbili, kisukari cha kupanda aina ya kwanza na cha aina ya pili, mtu mwenye dalili za awali za kupanda kwa sukari ila bado hana sifa za kuitwa anakisukari, kisukari chake huweza kudhibitiwa, na mtu huyu anaweza asiugue ugonjwa wa kisukari endapo atazingatia masharti ya chakula na mazoezi.
Kipo kisukari kinachotokea wakati wa ujauzito ambacho huitwa kisukari cha ujauzito, kisukari hiki huweza kuisha baada ya ujauzito au huweza kuendelea baada ya ujauzito
​
Aina za ugonjwa wa kisukari, Dalili, Vipimo na matibabu
​
Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote
​
​
Imeboreshwa 12.03.2020
​
Rejea​
​