​Namna ya kuishi maisha bora na ugonjwa wa kisukari
Madhara ya kisukari
Kisukari kina madhara ya muda mfupi na muda mrefu, mfano wa madhara ya muda mfupi ni kushuka kwa kiwango cha sukari mwiini, DKA na HHS na yale ya muda mrefu ni kufeli kwa figo, ganzi n.k.
Mongonjwa wa kisukari si rahisi kuhisi majeraha madogo yakitokea kwenye miguu kwa sababu ya kupungua kwa hisia za mfumo wa fahamu na hivyo huwa hatarini kupata maambukizi na majeraha makubwa.
Mazoezi yenye mpangilio maalumu hudhibiti kiwango cha sukari kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya 2,husaidia watu wasio na kisukari kujiondoa katika hatari ya kupata ugonjwa huu.