Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Dkt. Charles W, MD
9 Juni 2020 10:13:34
Mazoezi kwa wagonjwa wa kisukari
Mazoezi ya kuzingatia ratiba na yenye utaratibu maalumu huwa na faida kwa watu wenye kisukari aina ya 2, hata hivyo mazoezi huweza kusaidia watu wasio na kisukari kujiondoa katika kihatarishi cha kupata kisukari aina ya 2.
Jinsi gani mazoezi huzuia kupata kisukari?
Mazoezi yenye utaratibu maalumu na ya kuzingatia ratiba huweza kuongeza hisia za seli za misuli na maeneo mengine ya mwili dhidi ya homoni ya insulin, kwa kufanya hivi matumizi ya sukari ya glukosi huongezeka kuiondoa katika damu. Aidha kuongezeka kwa matumizi ya glukosi huzuia kuhifadhiwa kwa glukosi katika mwili kwa mfumo wa kuwa mafuta. Hivyo ukifanya zoezi unapunguza hatari ya kunenepa kupita kiasi
Ni aina gani ya mazoezi ufanye?
Kabla ya kujua aina ya mazoezi ya kufanya ni vema ukafahamu baadhi ya mambo kuhusu mazoezi, mambo haya yanaweza kukufungua ufahamu endapo ulikuwa hujui;
Kutoushughulisha mwili ni kihatarishi cha vifo kama vile mtu anayevuta sigara
Kiwango cha Uimara wa mwili kutokana na mazoezi huwa mtabiri mkubwa wa vifo vinavyosababishwa na kisukari
Mazoezi huweza kuwa matibabu imara ya kushusha sukari katika damu kuliko matumizi ya dawa,pia mazoezi huwa na madhara kidogo yasiyotarajiwa mwilini ukilinganisha na dawa za kunywa.
Mazoezi ya utaratibu maalumu, pamoja na kula mlo kamili wenye afya na kupunguza uzito huweza kuzuia hatari ya kupata kisukari aina ya 2 kwa asilimia 60.
Kumbuka kabla hujaanza mazoezi
Kabla hujaanza mazoezi hakikisha umefanya mambo haya
Kama hujafanya mazoezi siku nyingi, ongea na daktari wako kabla hujaanza kufanya mazoezi yoyote yale endapo mazoezi hayo yanatumia nguvu nyingi kuliko kutembea kawaida.
Hakikisha umevaa viatu vyenye ukubwa wa kukutosha na unajihisi vema ukiwa umevivaa
Usikilize mwili wako. Kama unapata maumivu ya kifua au unakosa pumzi wakati wa kufanya mazoezi ongea na daktari wako kwa msaada kamili.
Kama unatumia dawa ya insulin au madawa yanayoongeza uzalishaji wa insulin, hakikisha unapima kiwango cha sukari kabla, wakati na masaa kadhaa baada ya mazoezi ili kujua ni kwa jinsi gani mazoezi yanavyoathiri kiwango chako cha sukari katika damu.
Jaribu kubeba kitu cha kula kinachoweza kutibu kiwango cha chini cha sukari kwa haraka mfano vidonge vya glukosi, glukosi n.k ili endapo kiwango cha sukari kitashuka kuliko kawaida upate kutumia mara moja.
Sasa tuangalie aina ya mazoezi yanayotakiwa kufanyika, kwa ujumla mazoezi ya ukinzani na yale ya aerobiki huwa na umuhimu kwa watu wanaoishi na tatizo la kisukari
Mazoezi ya aerobiki
Ni mazoezi endelezi kama vile kutembea, kuendesha baiskeli, kuruka kamba, kucheza tenis. Sifa ya mazoezi haya ni kwamba huongeza upumuaji na mapigo ya moyo.
Mazoezi ya ukinzani
Mazoezi haya huambatanisha mazoezi ya kutumia vifaa vya mazoezi kama kunyanyua vitu vizito, kupiga pushup. Kama ukitaka kufanya mazoezi haya unatakiwa kuwasiliana na msahauri wako wa mazoezi kama daktari, mtaalamu wa mazoezi au mshauri wa kisukari ili akufundishe kwa namna gani uanze mazoezi haya taratibu bila kupata shida.
Muda gani unatosha kufanya mazoezi Kwa siku?
Malengo yako yanatakiwa kuwa kutumia angalau dakika 150 za mazoezi ya wastani au yale ya anaerobiki kwa wiki, mfano unaweza tumia dakika 30 kwa siku na ukafanya mazoezi kwa siku tano tu jumla utatumia dakika 150 kwa wiki.
Unatakiwa uanze taratibu, na uongeze mda wa mazoezi taratibu kwa dakika 10 kwa siku mpaka ufikie kiwango cha matarajio yako. Habari njema ni kwamba mazoezi aina tofauti ya mda mfupi ya angalau dakika 10 kwa kila aina ya zoezi, huwa mazuri kuliko zoezi aina moja linalotumia mda huo huo
Kama unaweza
Jaribu kuongeza zoezi la ukinzani kama kunyanyua vitu vizito kiasi mara tatu kwa wiki
Kumbuka
Mazoezi ya mwili na kisukari huweza kuwa magumu hasa kwenye kuchagua aina ya mazoezi kulingana na hali ya afya ya mwili wako, wakati wote ongea na daktari wako kuhusu aina gani ya mazoezi yanayokufaa wewe kulingana na hali yako ya kiafya.Ratiba ya mazoezi ya kutembea
Imeboreshwa
11 Desemba 2021 14:05:11
Uly clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote dhidi ya afya yako.
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.
Rejea za mada hii;
​
-
Tessier D, Meneilly GS. Diabetes management in the elderly. In: Gerstein HC, ed. Evidence-based diabetes care. Hamilton: BC Decker Inc., 2001, pg. 370–9.
-
Lipska KJ, De Rekeneire N, Van Ness PH, et al. Identifying dysglycemic states in older adults: Implications of the emerging use of hemoglobin A1c. J Clin Endocrinol Metab 2010;95:5289–95.
-
Crandall J, Schade D, Ma Y, et al. The influence of age on the effects of lifestyle modification and metformin in prevention of diabetes. J Gerontol A Biol Sci Med Sci 2006;61:1075–81.
-
Chiasson JL, Josse RG, Gomis R, et al. Acarbose for prevention of type 2 diabetes mellitus: The STOP-NIDDM randomised trial. Lancet 2002;359:2072–7.
-
DREAM (Diabetes REduction Assessment with ramipril and rosiglitazone Medication) Trial Investigators, Gerstein HC, Yusuf S, et al. Effect of rosiglitazone on the frequency of diabetes in patients with impaired glucose tolerance or impaired fasting glucose: A randomised controlled trial. Lancet 2006;368:1096– 105.
-
Inzucchi SE, Viscoli CM, Young LH, et al. Pioglitazone prevents diabetes in patients with insulin resistance and cerebrovascular disease. Diabetes Care 2016;39:1684–92.
-
Kronsbein P, Jorgens V, Muhlhauser I, et al. Evaluation of a structured treatment and teaching programme on non-insulin-dependent diabetes. Lancet 1988;2:1407–11.
-
Wilson W, Pratt C. The impact of diabetes education and peer support upon weight and glycemic control of elderly persons with NonInsulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM). Am J Public Health 1987;77:634–5.
-
Braun AK, Kubiak T, Kuntsche J, et al. SGS: A structured treatment and teaching programme for older patients with diabetes mellitus–a prospective randomised controlled multi-centre trial. Age Ageing 2009;38:390–6.
-
Fagan PJ, Schuster AB, Boyd C, et al. Chronic care improvement in primary care: Evaluation of an integrated pay-for-performance and practice-based care coordination program among elderly patients with diabetes. Health Serv Res 2010;45:1763–82.
-
McGovern MP, Williams DJ, Hannaford PC, et al. Introduction of a new incentive and target-based contract for family physicians in the UK: Good for older patients with diabetes but less good for women? Diabet Med 2008;25:1083–9.
-
Maar MA, Manitowabi D, Gzik D, et al. Serious complications for patients, care providers and policy makers: Tackling the structural violence of First Nations people living with diabetes in Canada. Int Indigenous Policy J 2011;21:http://ir.lib.uwo.ca/iipj/vol2/iss1/6. Article 6.Imechukuliwa 05.06.2020
-
Jacklin KM, Henderson RI, Green ME, et al. Health care experiences of Indigenous people living with type 2 diabetes in Canada. CMAJ 2017;189:E106– 12.
-
Chandler MJ, Lalonde C. Cultural continuity as a protective factor against suicide in First Nations Youth. Horizons 2008;10:68–72.
-
Oster RT, Grier A, Lightning R, Mayan MJ, Toth EL. Cultural continuity, traditional Indigenous language, and diabetes in Alberta First Nations: A mixed methods study. Int J Equity Health 2014;13:92. doi:10.1186/s12939-014- 0092-4.
-
Truth and Reconciliation Commission of Canada. Truth and reconcilliation commission of Canada: calls to action. Winnipeg, MB: Truth and Reconciliation Commission of Canada 2012. 2015. http://www.trc.ca/websites/ trcinstitution/File/2015/Findings/Calls_to_Action_English2.pdf.Imechukuliwa 05.06.2020
-
Yu CH, Zinman B. Type 2 diabetes and impaired glucose tolerance in aboriginal populations: A global perspective. Diabetes Res Clin Pract 2007;78:159– 70.
-
Gracey M, King M. Indigenous health part 1: Determinants and disease patterns. Lancet 2009;374:65–75.
-
Chronic Disease Surveillance and Monitoring Division, Centre for Chronic Disease Prevention and Control. Diabetes in Canada: Facts and figures from a public health perspective. Ottawa, ON: Public Health Agency of Canada, 2011 http://www.phac-aspc.gc.ca/cd-mc/publications/diabetes-diabete/facts -figures-faits-chiffres-2011/index-eng.php. Imechukuliwa 05.06.2020
-
Turin TC, Saad N, Jun M, et al. Lifetime risk of diabetes among first nations and non-first nations people. CMAJ 2016;188:1147–53.
-
Singer J, Putulik Kidlapik C, Martin B, et al. Food consumption, obesity and abnormal glycaemic control in a Canadian Inuit community. Clin Obes 2014;4:316– 23.
​