​Namna ya kuishi maisha bora na ugonjwa wa kisukari
Kudhibiti kisukari wakati unaumwa
Mgonjwa wa kisukari anapoumwa, kiwango cha huweza badilika au kubaki kile kile. Wakati huu unashauriwa kupima kiwango cha sukari mara nyingi kuliko kawaida mfano mara tatu hadi nne kwa siku.
Uzito mkubwa, kutoshughulisha mwili, historia ya kisukari kwa ndugu wa damu moja, kisukari cha ujauzito ni miongoni mwa vihatarishi vya kupata kisukari. Unaweza kudhibiti baadhi ya vihatarishi hivi kwa kufanya mazoezi na kuzingatia mlo.
Njaa ya mara kwa mara, kiu ya mara kwa mara, kukojoa sana na kupungua uzito ni miongoni mwa dalili za kisukari aina ya 2. Pima ili kuthibitisha kama una dalili hizi.