Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
Kisukari cha ujauzito
Kisukari cha ujauzito humaanisha nini?
Kisukari cha ujauzito ni tatizo la kutoshindwa kuhimili vyakula vya kabohaidrate na huanzia au huonekana kwa mara ya kwanza wakati wa ujauzito, tatizo hili huambatana na kiwango kikubwa cha sukari katika damu.
Je kisukari cha ujauzito huhusisha aina zote mbili za kisukari?
Ndio kisukari cha ujauzito huweza kuhusisha kisukari aina ya 1 na 2 ambacho hakikutambulika kabla ya ujauzito. Hata hivyo kutomudu kwa glukosi huwa ni kwa kiwango kidogo kabla ya ujauzito.
Jinsi gani kisukari cha ujauzito kinatofautishwa na kisukari aina ya 1 na 2?
Kisukari cha ujauzito kipimo cha Hb1C huwa kwenye kiwango cha kawaida
Kwenye wiki ya 6 baada ya kujifungua, kipimo cha uwezo wa kuhimili glukosi kwa kupewa gramu 75 za glukosi matokeo yake huwa ya kiwango cha kawaida kama cha watu wengine wasio na kisukari.
Kuna umuhimu gani wa kutambua kisukari cha ujauzito?
Kutambuliwa na tatizo la kisukari cha ujauzito huweza kusaidia kupambana na kisukari vema na kuzuia madhara wakati na baada ya ujauzito kwa mama na mtoto.
Kutambuliwa pia husaidia kutambua wagonjwa watakaofaidika na matibabu yasiyo dawa kama aina ya chakula, kupunguza uzito(kama una kitambi) na mpango wa mazoezi ya kila siku ili kuzuia madhara ya mbeleni na kupata kisukari kinachodumu.
Je ukubwa wa tatizo ukoje?
Ukubwa wa tatizo hutofautiana kati ya asilimia 0.15 hadi 15 ya ujauzito zote zinazotokea. Kwa sababu kisukari cha ujauzito hutokea kwa ukubwa tofauti tofauti ukitegemea idadi ya tafiti, makabila na taifa nchi, njia zilizotumika kuchunguza na wingi wa watu mahari palipofanyika utafiti, kujua ukubwa wa tatizo kwa ujumla huwa ni changamoto.
Madhara ya kisukari cha ujauzito ni yapi?
Wanwake wajawazito waliopata kisukari cha ujauzito huwa kwenye kihatarishi cha mda mfupi cha kupata matatizo ya ujauzito kama
-
Kifafa cha mimba
-
Uchungu kuja kabla ya mda
-
Maambukizi kwenye figo
-
Maji mengi kwenye chupa ya uzazi
-
Na kujifungua kwa upasuaji
-
Madhara ya muda mrefu ni kama kupata kisukari cha kudumu na madhara yake sana sana matatizo ya moyo
Nini madahara ya kisukari kwa kichanga tumboni?
Madahara ya mda mfupi ni
-
Hatari ya mtoto kuumwa na kufa
-
Mtoto kuwa mkubwa sana
-
Kukwana bega wakati wa kujifungua na hivyo kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida
-
Kujifungua kwa upasuaji
-
Mtoto kuzaliwa amekufa
-
Na matatizo ya uchakatajii seli yaliyo sawa nay ale ya kisukari cha kutegemea homoni insulin
Madhara ya muda mrefu ni;
-
Mtoto kuwa na kitambi
-
Kisukari cha ukubwa kuanza mapema
-
Matatizo ya kiakili na mijongeo
Je kuna madahara ya kiuumbaji yanaweza kutokea kwa kichanga tumboni kwa mama mwenye kisukari cah ujauzito?
Hapana. Kisukari cha kweli cha ujauzito huchelewa kutokea, kwenye miezi mitatu ya pili au mwanzoni mwa miezi mitatu ya mwisho huanza kuonekana. Kipindi hiki uumbaji wa viungo vya mwili unakuwa ushafanyika. Kama kisukari kikigunduliwa kwenye miezi mitatu ya kwanza inatakiwa kuthibitishwa kwa kipimo cha HbA1C kwamba ni kisukari aina ya 1 au 2 ambacho huweza kuathiri uumbaji kwa mtoto.
Kipimo gani kinachoshauriwa kupima kisukari cha ujauzito?
Kipimo kinachotakiwa hutegemea nchi na nchi na uongozi. Kwa sasa kipimo cha masaa matatu cha ustahimilivu wa glukosi (OGTT) huwa ni kipimo tambuzi kwa ajili ya kisukari cha ujauzito.
Kipimo hufanyikaje?
Kwa nchi zilizoendelea hufanyika kwa kuanza kutumia kutumia kwanza gramu 100 za glukosi. Ili kuweka standadi mazingira ya kipimo, unatakiwa kufunga masaa 8 wakati wa usiku kuamkia asubuhi lakini si zaidi ya masaa 14. Kutumia gramu 150 za kabohidrate kwa siku tatu kabla ya kipimo huwa lazima ili kupunguza majibu ya kukutwa huna kisukari wakati unacho kihalisia. Mgonjwa anatakiwa kupumzika kwa mda wa dakika 30 kabla ya kuanza kipimo na asivute sigara kwa masaa 12 kabla ya kipimo. Wakati wa kipimo mwanamke hatakiwi kuvuta sigara na anatakiwa abaki amekaa chini bila kujishungulisha na mambo mengine mazito(kazi). Baada ya damu ya kipimo kutolewa mgonjwa hupewa kunywa gramu 100 za glukosi ndani ya dakika 5. Ili kuendana na muda muda hunakiliwa wakati mgonjwa ameanza kunywa sukari hii. Damu huchukuliwa kwenye kwenye saa la 1, 2 na la 3. Baada ya kipimo, mgonjwa huweza kula mkate au chakula cha protini ili kuzuia kushuka kwa sukari .
Kiwango gani cha sukari hutumika kama rejea?
Viwango vya hivi karibuni vilivyoshauriwa na Coustan na Carpenter husema. Sukari isiyo kawaida huzidi 95mg/dL endapo mt ahajala kitu. Na baada ya isaa limoja baada ya kula haitakiwi kuzidi 180mg/dL bada ya masaa 2 isizidi 155gm/dL na masaa matatu isizidi 140gm/dL. Sukari isiyo ya kawaida hutambuliwa endapo vipimo viwili kati ay masaa hayo matatu vimeonekana kuwa vipo zaidi ya kipimo cha kawaida.
Mambo/jambo gani hurekebisha kiwango cha sukari mwilini?
-
Msongo; mawazo au kazi, maambukizi, michomo,mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito, ukuaji
-
Mda na aina ya insulin unayotumia
-
Chakula; mda na wakati wa kula
-
Mazoezi; aina na mda wa kufanya
Mazoezi huwa na mchango gani katika kurekebisha kisukari cha ujauzito?
Mazoezi hufanya kazi kubwa sanakurekebisha kisukari cha ujauzito. Misuli mikuu hutumia sukari kwa wingi ikitegemea aina ya mazoezi unayofanya. Matokeo huweza kuwa ya haraka hata kwa kutembea tu au kufanya kazi kwa masaa machache kama kuogelea. Inashauriwa kwa wanawake wajawazito ambao hawajapewa marufuku kufanya mazoezi wafanye mazoezi kama moja ya matibabu ya kisukari. Matokeo ya mazoezi huwa mazuri na husaidia kwenye afya ya moyo na mishipa ya damu kuliko kwa wanawake wanaozingatia chakula tu. Matokeo ya mazoezi huanza kuonekana wiki 4 baada ya ufundishwa na kufanya mazoezi na husaidia ini kuondoa sukari na utumiaji wa seli. Mazoezi wakati mwingine huweza kusababisha mtu kuacha kutumia insulin kwa baadhi ya wanawake wenye kisukari cha ujauzito.
Wakati gani insulin hutumika kama matibabu ya kisukari cha ujauzito?
Matumizi ya insulin kwenye kisukari cha ujauzito huwa si ya haraka. Kama kiwango cha kawaida kisipofikiwa ndani ya wiki 1 au 2 kwa kuzingatia chakula na mazoezi, matumizi ya insulin kwa kuchoma chini ya ngozi huanza. Aina ya insulin inayotakiwa kutumika uchaguzi hutegemea sehemu na sehemu. Baadhi ya mamlaka hushauri insulin inayofanya kazi haraka kama NPH au inayofanya kazi mda mrefu kama lente itumike wakati wa asubuhi au jioni au vipindi vyote. Baadhi ya taasisi zinataka itumike insuli inayofanya kazi mda mfupi iunganishwe na ile inayofanya kazi mda mrefu. Aina zote za uchaguzi ni njema ila tu kiwango cha sukari kifikie kila cha kawaida.
Wagonjwa wanaotibiwa na insulin wanatakiwa waambiwe umuhimu wa chakula na mda wa kutumia dawa, sana sana baada ya kula waambiwe chakula wanachotakiwa kula ni kipi. Tafiti nyingi zimeonyesha matokeo mazuri ya matibabu kwa kutumia insulin.
Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020
ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;