top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

 

Kizunguzungu

 

Kizunguzungu ni nini?

​

Kizunguzungu ni hali ya kuhisi kama unazimia au kukosa kuhimili kusimama. Miongoni mwa watu wazima wenye umri wa miaka 60 asilimia ishirini yao wamewahi kupata kizunguzungu na kuathiri utendaji kazi wao.

​

Watu huelezea kizunguzungu  kama;

 

  • Kichwa kuwa chepesi kama vile unataka kufa

  • Kukosa uwiano unapokuwa umesimama

  • Kuona kama unazunguka au vitu vilivyokuzunguka vinazunguka

  • Kuelea, kuogelea au kichwa kuwa kizito

 

Mambo gani muhimu kumweleza daktari wako kuhusu kizunguzungu?

​

Kizunguzungu mara nyingi hutokea kwa muda na hutoweka bila matibabu. Unapokuwa unaongea na daktari kuhusu dalili unazopata jitahidi kumwelezea nini kinachotokea na nini huamsha na hali hiyo inakaa kwa mda gani, hayo yatasaidia kumpa tetesi ni nini kinachosababisha.

​

​

Visababishi vya kizunguzungu

 

Visababishi vya kizunguzungu hutofautiana kutokana na dalili ambata. Huweza kusababishwa na homa ya mwendo-homa unayopata wakati upo kwenye mwendo ukiwa unasafiri kwenye gari ama ndege n.k

 

Au huweza kusababishwa na mvurugiko ndani ya sikio, maambukizi, ugonjwa wa moyo kukosa damu, madhara ya dawa, hofu iliyopitiliza au hali nyingine. Wakati mwingie kisababishi huwa hakijulikani.

​

Kizunguzungu, ikiwa pamoja na vertigo-kuhisi kelele masikoni, kama vikitokea bila dalili zingine  huwa mara nyingi haziashirii dalili za kiharusi.

 

Baadhi ya visababishi vya kizunguzungu ni kama;

 

Matatizo ndani ya sikio

 

 

Kupungua kwa damu kwenye sikio

​

  • Kutokana na kuganda/kuziba kwa mishipa ya damu

  • Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo

  • Mapigo ya moyo yasiyo na utaratibu

  • Shinikizo la damu kushuka chini unaposimama

  • Kiharusi

  • Kiharusi mpito(TIA)

 

Baadhi ya dawa zinazosababisha kizunguzungu

​

 

Visababishi vingine vya kizunguzungu ni;

 

​

​

Soma zaidi kuhusu shambulio la kizunguzungu wakati wa kulala au kukaa au kusimama kwa kubofya hapa

​

Bofya kila kisababishi kusoma zaidi au kutafuta kwenye kiboksi juu ta tovuti hii kilichoandikwa 'Tafuta chocote hapa...'

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia kitufe cha  'mawasiliano yetu' au bofya 'Pata tiba' chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshwa, 17.06.2021

​

​

Rejea za mada hii;

​

  1. MSD manual. Dizziness and Vertigo. https://www.msdmanuals.com/home/ear,-nose,-and-throat-disorders/symptoms-of-ear-disorders/dizziness-and-vertigo. Imechukuliwa 28.11.2020

  2. American Academy of Otolaryngology. Dizziness and motion sickness. https://www.entnet.org//content/dizziness-and-motion-sickness. Imechukuliwa 28.11.2020

  3. Flint PW, et al. Peripheral vestibular disorders. Cummings Otolaryngology. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.11.2020

  4. Bope ET, et al. Dizziness and vertigo. In: Conn's Current Therapy 2018. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.11.2020

  5. Branch WT, et al. Approach to the patient with dizziness. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.11.2020

  6. American Academy of Orthopaedic Surgeons. Heat injury and heat exhaustion. http://orthoinfo.aaos.org/topic.cfm?topic=A00319. Imechukuliwa 28.11.2020

  7. Moskowitz HS, et al. Meniere disease. https://www.uptodate.com/contents/search. American Academy of Orthopaedic Surgeons.

  8. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. Migraine information page. https://www.ninds.nih.gov/Disorders/All-Disorders/Migraine-Information-Page. American Academy of Orthopaedic Surgeons.

bottom of page