Imeandikwa na daktari wa ULY clinic
Koma
Koma ni neno la kitiba linalotumiwa na ULYCLINIC, neno hili lilitokana na neno tiba “Coma” ambalo mwanzo wake lilikuwa neno la Kigiriki “koma” likimaanisha “hali ya kuwa kwenye usingizi mzito”
Koma ni hali ya kutojitambua ambapo mtu huwa anaishi lakini hawezi kuitikia kichocheo.
Koma husababishwa na magonjwa ndani ya mfumo wa fahamu wa kati na hali zinazoathiri utendaji kazi wa mfumo huu wa kati.
Magonjwa yanayoweza kusababisha koma ni kama vile;
-
Uvimbe kwenye ubongo
-
Jeraha kwenye ubongo
-
Maambukizi ya uti wa mgongo
-
Madhaifu ya kimetaboliki kama kisukari, ketoasidosisi
-
Kiwango kikubwa cha sodium kwenye damu
-
Kiwango kikubwa cha kalisiamu kwenye damu
Kunywa sumu- mfano kunywa
-
Pombe nyingi kupitiliza
-
Madawa ya kulevya
-
Dawa za kuzuia degedege
-
Dawa jamii ya antihistamine
-
Benzodiazepine
-
Digoxin
-
Sumu ya metali nzito
-
Haidrokabon
-
Barbiturate
-
Insulin
-
Lithium
-
Organofosfate
-
Phencyclidine
-
Phenothiazine
-
Salicylates
-
Dawa za jamii ya tricyclic antidepressants
-
Mshituko
-
Haipoksia
-
Shinikizo la chini la damu
-
Arizimia
Koma wakati mwingine humaanisha kipindi cha mtu kuwa macho lakini kuwa na hali ya kutotambua mazingira aliyopo.
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba