Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
13 Agosti 2023, 09:12:38
Konstipesheni
Konstipesheni ni hali ya kupitisha kiasi kidogo cha kinyesi kigumu, kikavu na mara nyingi chini ya mara tatu kwa wiki.
​
Baadhi ya watu hudhani wana konstipesheni endapo hawapati choo kila siku, hata hivyo hakuna vigezo vya kusema ipi ni tabia ya kawaida ya mfumo wa chakula wa mtu. Ni vema kufahamu tabia ya mfumo wako wa chakula ili kukiwa na mabadiliko ndipo iwe rejea kama una konstipesheni au la.
​
Visababishi vya konstipesheni
Konstipesheni ni moja ya lalamiko kubwa la kwenye mfumo wa chakula. Visababishi vinaweza kuwa pamoja na;
​
Hali na tabia ya Maisha
​Mfano wa hali na tabia za kimaisha zinazosabaisha konstipesheni ni;
Kutokula nyuzinyuzi za kutosha kutoka kwenye chakula
Mazoezi
Vinywaji
Kubadilisha Maisha au ratiba
Kusafiri
Uzee
Matumizi makubwa ya dawa za kulainisha tumboÂ
Kujinyima kwenda choo wakati wa kuhisi haja kubwa
​
Matumizi ya Dawa
Mfano wa dawa zinazoweza kusababisha konstipesheni ni pamoja na;
Codeine
Opioid
Antasidi zenye aluminiamu
Antispasmodics
Antidepresant
Nyongeza ya madini chuma
Dawa za kupunguza maji mwilini(diuretics)
Dawa za kutibu kifafa
Â
Magonjwa katika mifumo ya mwili
​Mfano wa magonjwahayo ni kama yalivyoorodheshwa hapa chini katika kila mfumo.
Magonjwa ya utumbo mpana na puru kama vile;
Kuziba kwa utumbo
Makovu
Divatikulosisi
Uvimbe
Striktcha
Sindrome ya iritabo baweli
Ugonjwa wa Hirschsprung
​
Magonjwa ya mfumo wa fahamu kama vile;
Sclerosisi
Ugonjwa wa Parkinson
Jeraha kwenye uti wa mgongo
Siudo-obstruksheni
​
Magonjwa ya kimetaboliki kama vile;
Madhaifu ya tezi ya thairoidi
Yuremia
Magonjwa ya mfumo wa kinga au mfumo wa immunolojia kama vile;
Amailoidosis
Lupasi
Sclerodema
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
13 Agosti 2023, 09:12:38
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Kamusi ya kiingereza ya tiba ya oxford
2. Medical problem in dentistry na crispian sculy toleo la 6
3. ULY CLINIC Haja ngumu
4. ULY CLINIC kinyesi cha mbuzi.