top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

​

Ni nini ufanye ili uishi maisha bora zaidi?

​

Ili kuwa na maisha bora ya kiafya ni vema ukazingatia mambo yafuatayo

​

Fanya mazoezi

 

Ili uwe na afya bora, huna budi  kufanya mazoezi, kwa kufanya mazoezi unaweza kujiepusha na magonjwa mengi. Mazoezi hujenga misuli ya mwili na kuongeza kinga ya mwili dhidi ya maradhi, kupunguza kiasi cha mafuta  na  pia husaidia mzunguko wa damu uwe mzuri na kukinga dhidi ya magonjwa ya moyo.

​

Kusoma kuhusu mazoezi na afya bonyeza hapa

​

Tumia maji safi na salama 

 

Mwili wa binadamu umeundwa kwa kiasi kikubwa cha maji kwa asilimia 60 kwa mtu mzima na asilimia 70 kwa watoto, hivyo mtu hana budi kunywa maji safi na salama kila siku ili aweze kuepuka magonjwa mbalimbali yanayoweza kupatikana kwa kutokunywa au kunywa maji yasiyo salama. Maji pia yana umuhimu wa kutoa sumu mbalimbali mwilini kwa njia ya mkojo na kinyesi. Kiwango kinacho pendekezwa ni kunywa lita  1 1/2 (lita moja na nusu) kwa siku kwa mtu mzima ambaye hajafanya kazi nzito na si kwamba kiwango hicho ndo mwisho ila mtu anaweza kunywa maji mengi zaidi endapo anafanya kazi nzito ili kurudisha kiwango kinachokuwa kikipotea kwa njia ya jasho au pumzi inayotoka wakati wa kazi

​

Mtu anapopungukiwa na maji mwilini hupata dalili za kiu, midomo kukauka, kichwa kugonga, kuhisi uchovu, au kuchokachoka  na akipungukiwa kwa kiasi kikubwa hupata dalili mbaya zaidi kama kuzimia n.k

 

Kumbuka kuna baadhi ya wagonjwa wanatakiwa wadhibiti kiwango cha maji wanayokunywa kama vile wagonjwa wa moyo ulioferi na nephrotic syndrome

 

Soma kuhusu umuhimu wa maji ya moto kwa kubonyeza hapa

​

Mwanga wa jua

 

Mwanga wa jua ni wa umuhimu sana kwa binadamu kwa sababu husaidia katika utengenezaji wa vitamin D mwilini kupitia ngozi, mwanga unaoshauriwa ni ule wa asubuhi na mapema. Vitamini D hutumika katika utengenezaji na uimarishaji wa mifupa na pia huua vimelea wanaosababisha maradhi, ndio maana binadamu anapaswa kuishi katika nyumba yenye madilisha makubwa yanayongiza mwanga wa jua na hewa safi pia unatakiwa kujua kuna hasara za kukaa katika mwanga wa jua kwa baadhi ya watu(watu wenye ulemavu wa ngozi- albino, wanaojikirimu ngozi na watu wenye ,maambukizi ya VVU) kama vile kupata saratani ya ngozi kutokana na kupigwa na jua kali hivyo ni muhimu kukaa katika mwanga wa jua usio mkali hasa kipindi cha asubuhi kabla ya saa nne asubuhi

 

 

Kuwa na kiasi

 

Kiasi ni ile hali ya kutumia vitu visivyo na madhara kwa kiwango kinachohitajika na kujiepusha au kuacha kabisa matumizi ya vitu vinavyodhuru mwili. Kiasi katika suala la kula ni la umuhimu sana kwa afya ya mtu na kinyume chake ni kuharibu afya ya mtu. Tabia za ulevi wa kupindukia, uvutaji wa sigara , madawa ya kulevya hazina budi kuachwa kwa ajiri ya mtu kupata afya njema ya sasa na baadae.

​

Kula mlo kamili kutoka kwenye makundi matano ya chakula

​

Kuendelea kusoma kuhusu chakula na mlo kamili bonyeza hapa

 

​

Kusoma kuhusu namna ya kupima uimara wa mwili wako bonyeza hapa

bottom of page