Imeandikwa na ULY CLINIC
​
Umri wa ujauzito
​
Umri wa ujauzito(mimba) ambao hupimwa katika wiki unaweza kutambuliwa kwa njia mbalimbali zinafahamika. Siku ya kwanza kuhudhuria kliniki ya ujauzito, muuguzi wako atakuuliza kuhusu tarehe ya mwisho kuona siku zako au damu ya hedhi, na kisha atatumia tarehe hiyo ili kuweza kukokotoa tarehe yako ya kujifungua pamoja na umri wa ujauzito katika wiki. Hata hivyo utafanyiwa kipimo cha tumbo la ujauzito ili kuona una umri gani.
Njia za kutambua umri wa ujauzito
​
Njia zinazoweza kutambua umri wa ujauzito wako ni pamoja na;
-
Kukokotoa kwa kutumia tarehe ya mwisho kuona damu ya hedhi ya mwisho
-
Kutumia kimo cha ujauzito
-
Kipimo cha picha ya ultrasound
​
Ni njia gani sahihi ya kutambua umri wa ujauzito?
​
Licha ya kuwa na njia nyngi za kutambua umri wa ujauzito, njia sahihi na ambayo haibadiliki ni ya kukokotoa kutoka kwenye tarehe ya mwisho ya kuona hedhi ya mwisho. Hata hivyo njia hii haitakuwa sahihi endapo umesahau au haukumbuki vema tarehe hiyo. Njia ya kipimo cha Ultrosound ni nzuri zaidi endpo itafanyika katika kipindi cha kwanza cha ujauzito yaani miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Endapo kipimo cha ultrosound kitafanyika miezi mitatu ya mwisho kabla ya kujifungua, majibu ya kipimo huwa si sahihi kwani huongeza au kupunguza wiki kuanzia 2 hadi tatu. Hivyo hivyo njia ya kukipa kimo cha mimba huwa sahihi kipindi cha miezi sita ya mwanzo, huku matumizi ya njia hii kipindi cha karibia na kujifungua hutoa majibu yasiyo sahihi
​
Kipimo kwa kutumia tarehe ya mwisho kuona siku zako
​
Chini ya maelezo haya, utaweza kufahamu umri wa ujauzito wako katika wiki endapo unakumbuka tarehe ya kwanza ya siku ya mwisho kuanza kuona siku zako. Tafadhari tumia kikokoteo chini ya maelezo haya kukokotoa umri wa ujauzito wako.
Maelezo kuhusu majibu ya kikokoteo cha umei wa ujauzito na tarehe ya kujifungua hapo juu
​
Utakapotumia kikokoteo hicho hapo juu, utapata majibu kwenye mistari mitatu au hadi minne ya majibu ambayo yameandikwa kwa lugha ya kiingereza. Majibu hayo hutafsiriwa hivi kutoka mstari wa kwanza hadi wa tatu au nne.
​
Mstari wa kwanza unamaanisha kwamba, endapo hujuapata mimba utaingia hedhi inayofuata kuanzia tarehe ilioonyeshwa hapo juu.
​
Mstari wa pili unamaanisha kuwa endapo huna ujauzito tarehe yako ya siku za hatari inatarajiwa kuwa kati ya tarehe zilizoorodheshwa kwenye mstari wa pili
​
Mstari wa tatu unamanaisha, endapo umepata ujauzito tarehe yako ya matazamio ya kujifungua itakuwa kwenye tarehe hiyo iliyotajwa kwenye mstari wa tatu
​
Msatari wa nne ambao wakati mwingine hauonekani kwenye baadhi ya tarehe utakazoingiza unamanisha, endapo umepata ujauzito, ujauzito wako utakuwa na umri wa wiki zilizotajwa hapo kwenye mstari wa nne.
​
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi baada ya kusoma makala hii.
​
​
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga simu au bonyeza 'Pata Tiba' kupitia neno Pata Tiba chini ya tovuti hii. au Bonyeza hapa
​
Imeboreshwa, 23.01.2021
​
Rejea za mada hii,
​
-
JOHN HOPKINS https://www.hopkinsmedicine.org/health/wellness-and-prevention/calculating-a-due-date. Imechukuliwa 21.02.2020
-
Modified Naegele’s Rule for Determination of the Expected Date of Delivery Irrespective of the Cycle Length.
-
PDF. http://applications.emro.who.int/imemrf/med_j_cairo_univ_1994_62_1_39.pdf.Imechukuliwa 21.02.2020
-
Maswali na majibu kutoka kwa wateja wa
-
ulyclinic. https://www.ulyclinic.com/forum/majadiliano-na-wataalamu/nawezaje-kufahamu-tarehe-yangu-ya-kujifungua-endapo-nimesahau-tarehe-ya-mwisho-kuona-damu-ya-hedhi. Imechukuliwa 27.05.2020
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
​