top of page

Unaweza bofya ili kusoma zaidi kuhusu huduma ya kwanza kwenye mada hizi;

 

Kupaliwa

Aliyevunjika

Namna ya kufanya CPR

Kung'atwa nyoka

Aliyezama maji

Kuungua

Kupigwa shoti

Shambulio la moyo

Dhuriwa na sumu

Huduma ya kwanza kwa mtu aliye n’gatwa na nyoka

Imeandikwa na daktari wa uly clinic

Kung’atwa na nyoka huchangia katika vifo na ulemavu kwa binadamu sana sana maeneo ya bara la asia, amerika na afrika haswa katika nchi zilizo karibu na jangwa. Nyoka wenye sumu wapo sehemu mbalimbali katika duniani, wapo nyoka aina kadhaa na dalili nyingi zinazotokana na kung’atwa na nyoka hufanana fanana.

Dalili za mtu aliye ng’atwa na nyoka

 

Dalili ya kungatwa na nyoka kubwa huwa ni alama za mikwaruzo kutokana na kung'atwa na maumivu

Huduma ya kwanza kwa mtu aliye ng’atwa na nyoka

Madhumuni ya huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka hulenga kuzuia sumu ya nyoka kusambaa kwenye mwili na kupoteza mda kabla ya kumfikisha aliyejeruhiwa katika kituo cha matibabu

Mambo ya msingi ya kuzingatia ni

Mwondoe mgonjwa katika eneo lenye nyoka. Mtulize mgonjwa na apumzike na atulie katika bila kujitikisa katika eneo ulilomuweka

Jaribu kumtambua aina ya nyoka ikiwa tu kuna usalama kwa mgonjwa na wewe, na ikiwa hakutamchelewesha mgonjwa kufika katika kituo cha huduma za afya. Unaweza kupiga picha nyoka ukiwa mbali  kwa usalama hata kama nyoka amekufa mda mfupi.

Vua vipuli kwenye maeneo yaliyojeruhiwa, ikiwa mguu wa kulia au kushoto au mkono, ondoa vipuli hivyo katika maeneo hayo. Viatu pia viondolewe na ikiwa ananguo zilizobana kiasi kwamba kusababisha mzunguko wa damu usiwe mzuri ondoa nguo hizo. Nguo zisizobana acha kama zilivyo.

Tuliza eneo lililo jeruhiwa katika pozi salama. Eneo lililo jeruhiwa linaweza kuwekwa kwenye usawa wa moyo endapo nyoka hana sumu inayodhuru mishipa ya neva, au kuwekwa chini ya usawa wa moyo endapo nyoka ana sumu inayodhuru mishapa ya neva

Funga mguu au mkono na kitu kigumu kisichopinda kama mbao, kipande cha mti n.k katika maungio ya miguu ili kuzuia eneo hilo kujikunja kwa kufanya hivi

  • Weka kipande cha mti nyuma ya mguu ili kuzuia goti kujikunja na kiwiko cha mguu

  • Funga mkono ujikunje mbele ya kifua na kamba izunguke shingoni kama kwenye picha zinavyoonekana hapo chini

Msafilishe mgonjwa kwenye kituo cha huduma za afya haraka iwezekanavyo

Mzuie mgonjwa kutembea kwa sababu kukunja maungio misuli kufanya kazi husababisha sumu isambae zaidi mwilini.

Usikichokoze kidonda, isipokuwa endapo unataka kuweka bandaji  kwa kutumia mgandamizo kidogo kwenye kidonda na endapo unataka kusafisha kidonda kwa maji ikiwa mda wa kumsafilisha mgonjwa mpaka kituo cha afya utakuwa kidogo sana

Imeboreshwa mara ya mwisho 16.03.2020

Rejea

bottom of page