Imeandikwa na daktari wa ULY clinic
Uvimbe kwenye ulimi
Uvimbe kwenye ulimi unaweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali ambayo yameorodheshwa hapa chini.
-
Kuvimba kwa tezi za ulimi mfano kuvimba papilla za ulimi, kuna aina mbalimbali za papilla kwenye ambazo ni ulimicircumvallate (or vallate), fungiform, filiform na foliate. Papilla zote kwenye ulimi huwa na tezi za kuhisi radha ya chakula isipokuwa papilla za foliate. Angalia kwenye picha kuona maeneo ambayo kuna tezi hizi za papilla.
-
Fibroma
-
Papilloma
-
Uvimbe maji wa lymphangioma
-
Ranula
-
Mucocele
-
Kuvimba kwa mishipa ya damu ya ulimi
-
Saratani
-
Lympangioma
Makala hii imezungumzia uvimbe wa fibroma.
Uvimbe wa fibroma ni uvimbe usio saratani, hutokea sana na hutokana na mwitikio wa mwili dhidi ya uchokozi kwenye kinywa. Kwa jina jingine huitwa uvimbe wa majeraha, au polipu kwenye ulimi. Huweza kutokea kwenye ulimi/ kuta za ndani ya mashavu au kwenye fizi.
Vihatarishi vya kupata fibroma ni nini?
-
Uvimbe wa fibroma hutokea sana kwa watu wazima lakini hata hivyo hutokea kwenye umri wowote ule
-
Hudhuru asilimia 2 ya watu wazima
Visababishi
Husababishwa mara nyingi na uchokozi kwenye ulimi unaosababishwa na kujing’ata ulimi, kujikwangua na jino lililopasuka au kutobolewa na vifaa mbalimbali vinavyovaliwa kinywani.
Dalili
-
Ulimi huwa na nyororo na mgumu kama vile unavyohisi ukishika kilele cha pua
-
Huwa na rangi inayofanana na sehemu zingine za ulimi lakinipia huweza kuwa na rangi iliyopauka au rangi nyeusi
-
Kuta za kipele zinaweza kupata vidonda hvyo kupata makovu
-
Huweza kupata umbo kama la kipele mshikizo au kuwa kama kipele kilicho sehemu ya ulimi kama inavyoonekana kwenye picha
-
Hutokea sana pembezoni mwa ulimi kwenye usawa ambapo meno ya chini na juu yanapokutana, maeneo mengine ni pamoja na ndani ya kuta za mashavu, kwenye fizi na mdomo wa chini
-
Huwa hazisababishi dalili zozote zile
-
Huweza kukua ndani ya wiki au miezi kadhaa ili kufikia ukubwa wa kipenyo cha sentimita 1, hata hivyo huweza kukuwa zaidi ya hapa
-
Uvimbe wa fibroma huwa haubadiliki kuwa saratani
Namna gani ya kutambua tatizo
Ugonjwa utatambuliwa kwa daktari kuangalia uvimbe huo na kuushika, pamoja na kukuuliza historia ya tatizo hilo. Kinyama kinaweza kukatwa ili kupimwa ili kutofautisha uvimbe wa fibroma na vimbe zingine au kuuondoa uvimbe kabisa.
Je uvimbe wa fibroma ndani ya kinywa unaweza kupotea bila tiba?
Jibu ni hapana, uvimbe hauwezi kupotea bila matibabu
Matibabu ya fibroma
Matibabu endapo yatahitajika, uchaguzi wa pekee ni kuondoa kwa njia ya upasuaji. Uvimbe unaweza kutokea tena baada ya upasuaji endapo chanzo cha uchokozi wkenye ulimi kitaendelea.
Imeboreshwa mara ya mwisho, 24.06.2020
Endapo umesoma na kuona kuwa una tatio hili, ni vema ukawasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile.
Rejea za mada hii
-
Oral fibromas and fibromatoses. Medscape Reference. https://emedicine.medscape.com/article/1080948-overview. Imechukuliwa 24.06.2020
-
Periodontics. AAP. https://aap.onlinelibrary.wiley.com/doi/abs/10.1902/cap.2012.120069. Imechukuliwa 24.06.2020
-
RDH. Fibroma. https://www.rdhmag.com/pathology/oral-pathology/article/14173234/oral-pathologythe-fibroma-breaking-a-chronic-habit. Imechukuliwa 24.06.2020
-
Stoopler ET, Alawi F. Clinicopathologic challenge: a solitary submucosal mass of the oral cavity. Int J Dermatol 2008; 47: 329–331.