top of page
Jinshi ya kupima presha-ulyclinic.jpg

Imeandikwa na ULY CLINIC

​

Namna ya Kupima shinikizo la damu (presha)

 

Shinikizo la damu hufahamika na watu wengi kama presha hutokana na msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu. Msukumo huu huanzia kwenye moyo ambao umetengenezwa na misuli maalumu yenye uwezo wa kufanya kazi muda wote bila kuchoka. Ili kufahamu kuhusu afya ya moyo na mishipa ya damu, kipimo cha shinikizo la damu ni moja ya kipimo muhimu sana kufanyika angalau mara moja au mbili kwa kila  mwezi. Vipo vipimo vingine ambavyo unaweza  vifanya kila mwezi lakini kimojawapo ni kipimo cha kupima shinikizo la damu.

 

Kuna ina ngapi za shinikizo la damu?

 

Shinikizo la damu limegawanyika katika sehemu mbili, shinikizo la systolic na shinikizo la diastolic

  • Shinikizo la systolic hutokea pale moyo unaposinyaa ili kusukuma damu nje ya moyo kwend akwneye mishipa ya damu, shinikizo hili huwa kubwa zaidi kulilo lile la diastolic

  • Shinikizo la diastolic ni shinikizo la damu wakati moyo umelegea ili kupokea damu kutoka kwenye sehemu mbalimbali za  mwili kabla ya kuisukuma tena iende sehemu nyingine za mwili. Shinikizo hili mara nyingi huwa dogo kuliko lile la diastolic.

 

Shinikizo la damu hupimwa na kuandikwa katika uniti za milimita za mercury yaani mmHg

​

Ili kufahamu shinikizola damu unatakiwa kupima shinikizo la systolic na diastolic, baada ya kupata majibu, shinikizo la damu huandikwa kama sehemu yaani shinikizo la juu huwa ni lile la systolic na la chini huwa ni diastolic. Mfano umepima shinikizo la damu na kukuta shinikizo la systolic ni 120 na diastolic ni 60 hivyo shinikizo la damu litaandikwa 120/60mmHg)

 

Je ni shilingi ngapi kupima shinikizo la damu?

 

Vituo vingi vinapima shinikizo la damu bure kama sehemu ya kufanya watu wafahamu kuhusu shinikizo lao la kawaida na kutambua mabadiliko endapo yametokea. Hata hivyo unaweza kununua kipima shinikizo la damu na ukakaa nacho nyumbani hivyo kukitumia mara pale utakapohitaji.

 

Unaponunua chagua kifaa ambacho kinadumu, unauwezo wa kukitumia au unaweza kukitumia baada ya kufuata maelekezo.

 

Unahitaji nini ili kuweza kupima presha?

 

Ili kuweza kupima presha unahitaji  kuwa na kifaa cha kupimia shinikizo la damu vyenye majina tofauti kama blood presha machine, digital BP mashine, au sphygmomanometer. Unaweza kuhitaji kuwa na kifaa kinachoitwa stethoscope wakati unapima shinikizo la damu kwa kutumia sphygmomanometer.

 

Vifaa vya kupima shinikizo la damu vipo vya aina nyingi vya kidigitali na analogia. ULY CLINIC inashauri utumie vifaa vya analogia kwa sababu huwa havihitaji utaalamu mwingi nan i rahisi sana kutumia na kupata majibu haraka ukilinganisha na vifaa vya analogia ambavyo huhitaji uzoefu, hutumia muda. Hata hivyo endapo utaweza kujifunza kutumia vifaa vya analogia ni vema zaidi kwa kuwa majibu yake huwa hayabadiliki kama yale ya kidigitali.

 

Vifaa vya kidigitali huleta majibu yenye utofauti na majibu ya vifaa vya analogia endapo unatumia betri zilizoisha nguvu. Kifaa kinachotumia umeme wa moja kwa moja kutoka kwenye swichi huwa ni kizuri zaidi kwani umeme sawia huingia muda wote kwenye kifaa chako. Hivyo unashauriwa kutumia kifaa kinachotumia umeme wa swichi au tumia betri mpya kila baada ya kutumia betri(dura cell au zingine zinazodumu zaidi) kwa wiki mbili mfururizo wakati huo endapo hutumii hakikisha betri umezitoa kwenye kifaa chako ili zisiendelee kuisha.

 

Jinsi ya kupima shinikizo la damu

 

Unapokuwa unapima presha au shinikizo la damu mambo muhimu kukumbuka ni kwamba unatakiwa kupima zaidi ya mara moja, ULY CLINIC inashauri kupima mara tatu. Kwanini unatakiwa pima mara tatu? Jibu ni kwamba shinikizo la damu katika siku hubadilika badilika ikitegemea vitu mbalimbali kama vile mazingira ya baridi au joto sana, mazoezi, msongo wa mawazo, huzuni, maumivu n.k. Kupata vipimo vitatu vinaweza kutambua shinikizo lako halisi, usikubali kusema kwamba una shinikizo la juu kwa kipimo kimoja tu kwa siku, pima mara tatu au zaidi ili kuweza kutambua shinikizo lako halisi ni lipi. Ili kutambua shinikizo halisi utaona kwamba shinikizo la diastolic au systolic halitofautiani kwa zaidi ya mmHg 2 hadi 3 kati ya vipimo vitatu ulivyopima angalau masaa mawili au matatu zaidi.

 

Jambo jingine la kukumbuka, unapopima shinikizo la damu hakikisha umepumzika angalau kwa dakika tano endapo ulikuwa unatembea au kutoka kufanya mazoezi au kufanya shughuli yoyote ile, hii ni kwa sababu shinikizo la damu hupanda endapo umetoka kutembea ua kufanya kazi yoyote ile.

 

 

Namna ya kupima shinikizo la damu kwa kutumia kifaa cha sphygmomanometer

​

Ili kuweza kupima shinikizo la damu kwa sphygmomanometer hakikisha una  stethoscope pia na unafahamu kuitumia na kasha fuata hatua 11 zifuatazo;

​

  1. Muweke unayempima kwenye kiti

  2. Hakikisha mkono wa unayempima upo pembeni na umeegamia kwenye mkono wa kiti

  3. Funga kitambaa(cuff) ya kipimo chako kwenye mkono kiasi kwamba kikae katikati ya mkono yaani katikati kati ya kiwiko cha  mkono na bega linapoanzia.

  4. Hakikisha unapofunga kitambaa hufanyi kikaze au kuwa legevu kiasi kwamba kidondoke chenyewe maana hii italeta majibu yasiyo ya kweli

  5. Shika na  hisi mdundo wa mishia ya damu katika maeneo ya mbele ya kiwiko cha mkono unaopima shinikizo la damu mara baada ya kuyasikia sasa unaweza kuanza kujaza upepo kwenye kipimo chako

  6. Hakikisha upepo hautoki nje ya koko na mara unapohisi mdundo wa mishipa ya damu umeisha usiendelee kujaza upepo bali acha hapo hapo kasha

  7. Weka stethoscope kwenye eneo ambalo ulikuwa unahisi mdundo wa mishipa ya damu kisha vaa pia kwenye masikio na baada ya hapo,

  8. Fungua taratibu koki ya sphygmomanometer ili kuruhusu upepo utoke kwa kiasi cha mmHg 1-2 kwa sekunde huku ukisikiliza sauti kwenye stethoscope yako iliyowekwa masikioni, unaposikia sauti ya mdundo wa mishipa ya damu kwa mara ya kwanza hapo ndo shinikizo la diastolic, rekodi shinikizo hilo kichwani kasha

  9. Endelea kuruhusu upepo utoke taratibu mpaka sauti ya mdundo wa mishipa ya damu inapofika point ya kuisha kabisa kasha rekodi shinikizo hilo ambalo ndo litakuwa shinikizo la diastolic

  10. Baada ya hapo ruhusu upepo wote utoke na rekodi kwenye karatasi majibu yako

  11. Toa sphygmomanometer kwenye mkono wa mgonjwa kasha hifadhi vema kifaa chako.

 

Namna ya kupima shinikizo la damu kwa kutumia kipimo cha kidigitali

 

Kama ilivyotanguliwa kusemwa hapo awali , vipimo vya kidigitali ni rahisi kutumia na vipo vya aina tofauti. Endapo unatumia kifaa cha kupima shinikizo la damu ni vema kufahamu kifaa hiko kinatumiwa maeneo gani ya mwili.

 

Kifaa kinachovaliwa mkono wa mbele

​

Endapo kinatumia kwenye mkono wa mbele yaani kuvaliwa karibu na maungio ya kijanga cha mkono hakikisha kwamba mkono wa unayempima umejikunja katika nyuzi 45 na umeuweka katibu na usawa wa moyo endapo utachora mstari mnyoofu(angalia picha kwa rejea zaidi). Fuata hatua namba 1 haadi 4 hapo juu, kasha bonyeza kitufe cha start. Mara baada ya kujaza upepo na kuutoa kasha kuonyesha namba, rekodi majibu yako kwenye kitabu cha kumbukumbu kabla ya kukitoa na kukitunza sehemu salama kwa matumizi ya baadae.

 

Kifaa kinachovaliwa kwenye mkono

 

Endapo kifaa chako ni kile ambacho kinatakiwa kuvaliwa kwenye mkono yaani kati ya bega kiwiko cha mkono au mkono wa nyuma, fuata hatua namba 1 hadi 4 za hapo juu. Kasha bonyeza baton ya start na mashine inaposimama kuhesabu na kutoa namba rekodi majibu yako mara moja pembeni kasha kitoe kifaa chako na kukitunza.

 

Namna ya kutafsiri majibu ya vipimo

 

Baada ya kupima shinikizo la damu, ni vema ukafahamu majibu yako na kuwe kuyatafsiri ili endapo kuna hatua za kufuata uweze kuzifuata baada ya kushauriana na daktari wako. Shinikizo la damu linaweza kusemekana kuwa la kawaida, limepanda na limeshuka. Kwa namna nyingine husemekena kuwa una presha ya kawaida(shinikizo la kawaida), una presha ya juu(shinikizo la damu la juu) au una presha ya chini(shinikizo la chini la damu). Ili kuelewa zaidi angalia maelezo hapa chini;

 

  • Presha ya kawaida(shinikizo la kawaida): Endapo kipimo kimeonyesha presha yako ya systolic ipo chini ya 140mmHg na diastolic ipo chini ya 90

  • Presha ya juu(shinikizo la damu la juu): endapo presha yako ya systolic ni 140mmHg au zaidi  na ile ya diastolic  ni 90mmHg au zaidi

  • Una presha ya chini(shinikizo la chini la damu): Endapo shinikizo la damu la systolic lipo chini ya 90 na lile la diastolic lipo chini ya 60.

​

Imeboreshwa 23.4.2021

​

Rejea za mada hii

​

  1. NCBI. What is blood pressure and how is it measured.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK279251/#. Imechukuliwa 2.1.2021

  2. Kasper DL, Fauci AS, Hauser SL, Longo DL, Jameson JL, Loscalzo J. Harrison's Principles of Internal Medicine. New York: McGraw-Hill; 2015.

  3. American heart association. Monitoring-your-blood-pressure-at-home.https://www.heart.org/en/health-topics/high-blood-pressure/understanding-blood-pressure-readings/monitoring-your-blood-pressure-at-home. Imechukuliwa 2.1.2021

bottom of page