top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

 

Tatizo la Kichefuchefu na Kutapika sana  wakati wa ujauzito

​

Ni hali kali na inayoweza kutokea kwa mama mjamzito inayoambatana na kichefuchefu na kutapika sana au kwa namna nyingine ni kitendo endelevu cha kutapika wakati wa ujauzito kunakosababisha kupoteza uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito wa awali.

 

Huweza kupelekea kupoteza uzito, kuwa na lishe duni na kuharibika kwa usawia wa giligili, na kuharibika usawa wa kemikali mbalimbali mwilini.

 

Tatizo hili huambatana na kiwango kikubwa cha homoni ya HCG ambayo hutolewa kwenye kifuko cha mimba.

 

Ukubwa wa tatizo

 

Hutokea sana kwenye wiki 8 hadi 12 za ujauzito, na dalili hupotea wiki ya ishirini kwa wengi lakini asilimia 10ya wenye tatizo hili.

Asilimia 0.3 hadi 2 ya wanawake wanaopata mimba katika mwaka huathiriwa na tatizo hili.

 

​

Vihatarishi

 

Kuwa na ndugu mwenye tatizo hili kama dada, binti wa mama mwenye tatizo hili huwa kwenye hatari ya kupata tatizo hili.

  • Historia ya tatizo kwenye ujauzito ulipita

  • Mimba mapacha

  • Kuwa na hali ya kijeni inayoitwa triploidy na trisomy

  • Kuwa na ujauzito unaoitwa molar au kuwa na historia kwenye ujauzito uliopita

 

Wanawake  wenye historia hizi pia huweza kupata tatizo hili

  • Homa ya miendo

  • Kipanda uso

  • Magonjwa ya kiakili

  • Kisukari wakati wa ujauzito

  • Kiwango cha juu cha homoni ya thyroid

  • Upungufu wa vitamin B

​

Dalili

 

  • Kupoteza uzito zaidi ya asilimia 5 kwenye ujauzito

  • Kukaukiwa maji mwilini, kunakosababisha kuongezeka kwa kiwango cha ketoni na kupata choo kigumu

  • Lishe duni

  • Kubadilika kwa ladha ya chakula

  • Kuongezeka mara dufu hisia ya ubongo dhidi ya miendo

  • Kubadilika kwa homoni kwa haraka wakati wa ujauzito

  • Vitu vilivyomo kwenye tumbo kurudi juu ya kinywa

  • Msongo wa kimwili na hali

  • Kuvia damu kwenye macho

  • Kushindwa kufanya kazi za kila siku

  • Kuweweseka/ndoto za mchana

​

Matibabu

 

Nia ya matibabu ni kutibu dalili na kuwa makini kwenye kiwango cha maji kwenye damu. Kula chakula mara kwa mara kwa kiasi kidogo na kujizuia na vyakula vinavyosababisha kichefuchefu na kutapika huwa ni jambo la muhimu. Chai ya tangawizi imekuwa ikitumiwa zamani na hutoa uahueni sana. Matumizi ya vitamin B6 huwa ya msingi pia kwa kutibu dalili hizi kuna matibabu mengine ya kusisimua mishipa ya fahamu kupitia ngozi yanayoweza kufanyika kwenye baadhi ya hospitali hapa duniani.

 

Dawa za kuzuia kichefuchefu na kutapika hushauriwa kutumiaka endapo hakuna njia nyingine baada ya kupata giligili-maji ya kutosha kupitia mishipa. Dawa kama metroclopramide, phenothiazine na ondansetron ni dawa nzuri na huwa salama kipindi cha ujauzito. Dawa za  mishipa jamii ya steroid hutumika kwa wagonjwa ambao wameshindwa kusaidiwa na dawa za kuzuia kutapika.

​

Mwisho ednapo tatizo la kutapika ni sugu na limeshindikana kwa dawa unaweza kupewa chakula kwa njia ya mishipa hutumika kwa haswa kwa wagonjwa ambao wanashindwa kuwa na uzito unaotakiwa kwa sababu ya kutapika sana japokuwa wanapata matibabu.

​

ULY CLINIC inakukumbusha uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua zozote zile za kiafya

​

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

​

​

Soma zaidi kuhusu Kutapika kwa kubonyeza hapa

​

​

​

Rejea za mada hii

​

1. American pregnancy association. https://americanpregnancy.org/pregnancy-complications/hyperemesis-gravidarum/. Imechukuliwa 25.05.2020

​

2. Williams Obstetrics Twenty-Second Ed. Cunningham, F. Gary, et al, Ch. 49.
HER Foundation, www.hyperemesis.org.  Imechukuliwa 25.05.2020

 

3. Smith JA, et al. Treatment and outcomes of nausea and vomiting of pregnancy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 25.05.2020

 

4. Natural medicines used during pregnancy and lactation. Natural Medicines. https://naturalmedicines.therapeuticresearch.com. Imechukuliwa 25.05.2020​

 

5.American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG) Committee on Obstetric Practice. Committee Opinion No. 722: Marijuana use during pregnancy and lactation. Obstetrics & Gynecology. 

​

6.Vitamin B-6. Office of Dietary Supplements. https://ods.od.nih.gov/factsheets/VitaminB6-HealthProfessional/. Imechukuliwa 25.05.2020​

​

​

Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;

​

Kutapika sana ujauzitoni
bottom of page