Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Utangulizi
​
Haipahidrosis
​
​
Haipahaidrosis ni neno tiba linalomaanisha kutoa jasho kwa wingi kusiko kwa kawaida(kutokwa na jasho jingi), kusikohusiana na mazoezi au joto kali. Jasho hili linaweza kutoka sehemu Fulani tu katika mwili au mwili mzima. Neno tiba hili limetokana na neno ‘hidrosis’ ambalo ni neno la kigiriki na kilatini lenye maana ya ‘kutoa jasho’
​
Mtu anaweza kutokwa na jasho jingi kiasi kwamba likaharibu ubora wa maisha yake, jasho linaweza kuchuruzika au kulowanisha sehemu ya nguo au nguo yote.
​
Dalili
​
Dalili huwa ni;;
​
-
Kutokwa na jasho kupita kiasi wakati wa mazoezi na kutembea
-
Kutokwa na jasho zaidi ya watu wengine wakati upo kwenye hali ya hewa ya joto
-
Jasho kutoka sehemu mbili zinazofanana mwilini mfano makwapa yote, viganja vya mikono, miguuni
-
Kutokwa na jasho maeneo ya usoni, kanyagio la miguu, viganja vya mikono, miguuni au mikononi
​
Endelea kusoma kwa kubonyeza hapa chini
​
Utangulizi Visababishi matibabu Kumwona daktari
​
​
Imeboreshwa, 04.11.2020
​
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kw aushauri zaidi na tiba inayoendana na matakwa yako kabla ya kuchukua hatuaa yoyote ile
​
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri zaidi na Tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza Pata Tiba chini ya tovuti hii.
​
-
Hyperhidrosis. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/dermatologic-disorders/sweating disorders/hyperhidrosis. Imechukuliwa 04.11.2020
-
Smith CC, et al. Primary focal hyperhidrosis. https://www.uptodate.com/content/search. Imechukuliwa 04.11.2020
-
What is a heart attack? National Heart, Lung, and Blood Institute. http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/heartattack. Imechukuliwa 04.11.2020
-
Hyperhidrosis. https://www.merriam-webster.com/dictionary/hyperhidrosis. Imechukuliwa 04.11.2020