top of page

Huduma ya kwanza kwa mtu aliyevunjika

 

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

Inaweza kuwa vigumu kwa mtu asiye mtaalamu wa afya kutambua kama majeruhi amevunjika. Kama huna uhakika mtibu majeruhi kama mtu aliyevunjika

Kama amepoteza fahamu au kuvuja damu kwa wingi, unatakiwa kumpa huduma ya kwanza ya kuzuia damu kutoka kwa kuweka mgandamizo kwenye sehemu inayotoa damu na kufanya CPR. Soma kuhusu mada ya namna ya kumhudumia mgonjwa anayetokwa damu.

Endapo anajitambua, zuia au punguza maumivu au kuendelea kuumia kwa kutuliza sehemu iliyovunjika kwa kadri inavyowezekana mpaka afike hospitali

Ukishamaliza hivyo tafuta njia ya kumpleka hospitali, ikiwa ni kwa ambulance au kwa gari binafsi

Kama maumivu si makali sana msafilishe kwa njia ya gari la binafsi kwenda hospitali. Tafuta mtu wa kuendesha gari kama inawezekana ili wewe ukae na majeruhi

Piga simu namba 112 endapo

  • Majeruhi ana maumivu makali sana na anahitaji dawa za kuua maumivu, piga simu haraka lakini kumbuka usimtembeze, mwambie atulie hapo hapo endapo kuna usalama tu.

  • Unaona kwa macho yako kwamba amevunjika mguu, usiutingishe, acha  mguu kwenye hali jinsi ulivyoukuta

  • Unahisi atakuwa amevunjika mgongo

Usimpe majeruhi kitu chochote cha kula au kunywa kwa sababu anaweza hitaji kupewa dawa za usingizi/kaputi akifika hospitali kwa ajili ya kufanyiwa operation.

Unaweza kusoma Zaidi kuhusu huduma ya kwanza kwa kila aina ya kuvunjika kwa kubonyeza mada inayohusika

  • Kuvunjika kiwiko cha mguu

  • Kuvunjika mkono au kiwiko cha mkono

  • Kuvunjika pua

  • Kuvunjika kidole cha mguu

  • Kuvunjika mbavu

  • Kuvunjika nyonga

Toleo la 3

Imeboreshwa mara ya mwisho 17/12/2018

Unaweza bonyeza na kusoma kuhusu huduma ya kwanza kwa mtu aliye

 

Kupaliwa

Kuungua

Namna ya kufanya CPR

Kung'atwa nyoka

Aliyezama maji

Aliyevunjika

Kupigwa shoti

Shambulio la moyo

Dhuriwa ma sumu

bottom of page