Imeandaliwa na daktari wa ULY-Clinic
Kuvimba kwa mitoki-tezi la limfu (Lymphadenopathy)
Kuvimba kwa tezi za limfu au kwa jina jingine la mitoki mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakiteria au virusi katika tezi. Uvimbe wa tezi limfu kitiba huitwa Lymphadenopathy
​
Endapo kuvimba kwa tezi za limfu kumesababishwa na maambukizi, hali hii huitwa Lymphadenitits, kwa mara chache sana kuvimba kwa tazi za limfu huweza kusababishwa na saratani.
Tezi za limfu hufanya kazi za msingi katika kupambana na maambukizi dhidi ya bakteria virusi na magonjwa mengine. Maeneo ya msingi ambayo unaweza kuona tezi za limfu zimevimba ni shingoni, chini ya kidevu, kwapanina maeneo ya kinena.
​
Kwa baadhi ya wagonjwa, kusubiria muda fulani upite au kukanda kwa kutumia maji ya uvuguvugu husababisha kupotea kwa vimbe hizi. Matibabu ya hospitali ya kuvimba kwa tezi linfu hutegemea kisababishi, endapo kisababishi kimefahamika kikitibiwa uvimbe huondoka wenyewe.
​
​
Soma zaidi kuhusu Dalili na visababishi , matibabu bonyeza hapa
​
ULY clinic inakukumbusha uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ili inayodhuru afya yako.
​
​
Imeboreshwa 20.11.2020