top of page

Imeandikwa na madaktari wa ULY Clinic

Kuzimia wakati wa kukojoa

 

Utangulizi

Kuzimia wakati wa kukojoa, ni kuzimia wakati au mda mfupi baada ya kukojoa kunakosababishwa na kushuka kwa shinikizo la damu. Hali hii hutokea sana kwa wazee na hutokea sana wakati wa usiku baada ya kutoka kwenye usingizi mkali.

 

Kisababishi mara nyingi hakieleweiki vema lakini huhusiana na kutanuka kwa mishipa ya damu unapotoka kwenye usingizi na kuamka kwenye kitanda au unapokuwa unakojoa haraka. Hii huonekana kusabaisha kushuka kwa shinikizo la damu.

 

Mambo mengine yanayoweza kuchangia kuzimia wakati wa kukojoa ni kama

 

  • Pombe

  • Njaa

  • Kuchoka mwili

  • Kukaukiwa maji/kuishiwa maji

  • Magonjwa kama maambukizi kwenye mapafu

  • Matumizi ya dawa za moyo aina ya alpha blocke kwa wanaume ili kuzuia dalili za kuvimba tezi dume

 

Kujikinga na kuzimia wakati wa kukojoa.

 

Kuzimia wakati wa kukojoa hakutokei sana, mara kunapotokea daktari atatakiwa kuchunguza ni tatizo gani linalosababisha kuzimia huko.

 

Kujikinga na kuzimia huku hutegemea utambuzi visababishi vinavyopelekea kuzimia wakati wa kukojoa.

 

Baadhi ya mikakati unayoweza kumshauri ndugu ama jamaa mwinye tatizo na kutopata majeraha wakati wa kuzimia ni kama;

  • Punguza unywaji wa pombe

  • Kutoamka/toka kitandani ghafla kaa kwa mda Fulani kitandani na chezesha miguu na hakikisha hauna kizunguzungu ndo uamke

  • Kojoa ukiwa umekaa chini

  • Mwulize daktari wako kama dawa zozote unazotumia zinaweza kuwa zinachangia kwenye tatizo hili

  • Hakikisha sakafu ya nyumba yako kutoka kitandani hadi chooni ina kapeti ili kuzuia kujigonga kwenye sumenti ama kigae

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako sikuzote endapo umeona dalili yoyote inayoendana na wewe kabla ya kuchukua uamuzi unaodhuru afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia namba za simu au bonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Soma makala ingine kuhusu kuzimia bonyeza hapa

Soma kuhusu kuzimia kutokana na vasovago refleksi bonyeza hapa

Imeboreshwa mara ya mwisho 1.07.2020

Dalili na viashilia A-Z

Chagua herufi ya kwanza ya dalili au Kiashiria , mfano maumivu ya kichwa ambayo yapo kwenye herufi M kisha ingia na soma kuhusu maumivu ya kichwa

[A]  [B]  [C]  [D] [E]  [F]  [G]  [H]  [I]  [J] [K] [L] [M]  [N] [O]  [P]  [Q] [R]  [S]  [T ] [U]  [V ] [W]  [X ] [Y]  [Z] [#]

bottom of page