top of page
Kuzuia madhara ya kisukari
Kuzuia madhara ya kisukari
Imeandikwa na madaktari wa ulyclinic
Dakitari au mgonjwa wa kisukari anaweza kuzuia madhara ya kisukari kwa kufanya yafuatayo
-
Kupima HBA1c kila baada ya miezi 3 hadi 6
-
Kupima macho kila mwaka
-
Kupimwa kiwango cha protini kwenye damu
-
Kujichunguza miguu kuona kama kuna vidonda na kuvitunza na kupata matibabu kama vitakuwepo
-
Kupima shinikizo la damu linatakiwa liwe chini ya 135/80 au pungufu ya hapa kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo kutokana na kisukari
-
Kuwa kwenye dozi ya dawa ya statin ili kuzuia hatari ya kupanda kwa lehamu mbaya mwilini Low density lipoprotein cholesterol (LDL-cholesterol)
Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote
Imeboreshwa 12.03.2020
bottom of page