Maambukizi ya bacteria kwenye mfumo wa kizazi baada ya kujifungua
Imeandikwa na madaktari wa ulyclinic
Haya ni maambukizi bacteria kwenye via vya uzazi ambayo hutokea kama madhara baada ya kujifungua, bakiteria hawa hupitia milango ya uzazi(uke) na kuingia katika mfuko wa kizazi
Kwa sasa kumepungua kiwango cha watu wanaopata maambukizi baada ya kujifungua kwa sababu ya uboreshaji wa huduma na kupatikana ama kuwepo kwa dawa dhidi ya bakteria
Maambukizi haya hutokana sana na
1 maambukizi kwenye kuta za ndani ya mfuko wa kizazi
2. Maambukizi ya kuta za ndani na nje ya mfuko wa kizazi
3. Maambukizi ndani nje na via vinavyozunguka mfuko wa kizazi.
Bakiteria na fungus wenyeji katika milango ya uzazi –normal flora
Fngus aina ya candida albicans, bakiteria aina ya staphylococcus albus au aureus, bakiteria aina ya streptococcus, bakiteria E.coli na bacteroides na clostridium welchii kwa mara chache sana. Bacteria hawa hutawala maeneo ya milango ya via vya uzazi na hawaleti matatizo endapo uzazi umefanyika kwa kuzingatia usafi.
Mambo gani yanaweza usababisha kupata maambukizi ya wadudu hawa katika via vya uzazi na damu?
Wadudu hawa wanaweza kuanza kuleta madhara endapo kuna mambo yafuatayo;
1.Kubomoka kwa ute kati ya shingo ya uzazi na uke wakati wa kujifungua kawaida,
2. Kubadilishwa na kuwa kidonda kwa kuta za uzazi mahali ambapo kondo la nyuma lilikuwa limejishikiza
3. Kuvia kwa damu ndani ya kizazi maeneo kondo la nyuma linapojishikiza(damu huwa rafiki wa bakiteria kwa sababu huwafanya kupata chakula na kuongezeka)
Sababu zingine zinazoweza kuchangia ni kama vile
Wakati wa ujauzito kabla ya kujifungua;
-
Lishe duni kwa mama na upungufu wa damu,
-
kupata uchungu kabla ya siku za ujauzito kukamilika,
-
kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu kuanza, kuwa na ugonjwa sugu unaodhuru sana mwili,
-
kupasuka kwa chupa ya uzazi mapema zaidi ya masaa 18 kabla ya kujifungua.
Wakati wa kujifungua mambo haya yanaweza kuchangia pia
-
Kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara ukeni(kuwekewa vidole),
-
Kupasuka kwa chupa ya uzazi zaidi ya masaa 18 kabla ya kujifungua,
-
Kuishiwa maji mwilini wakati wa uchungu,
-
Jeraha wakati wa kujifungua kwa upasuaji, kupoteza damu nyingi wakati ama baada ya kujifunfungua,
-
Kubaki kwa mabaki ya kondo la nyuma katika mfuko wa kizazi,
-
kondo la nyuma kujishikiza karibu sana na uke,
-
Kujifungua kwa njia ya upasuaji
​
Imeandikwa 3/3/2015
Imeboreshwa 14/11/2018
​