Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Kabla ya kusoma makala hii kumbuka
​
ULY CLINIC inakushauri sikuzote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kujitibu mwenyewe. Epuka madhara unayoweza kuyapata kwenye kiungo hiki muhimu kwa kufanya hivyo.
​
​
Macho
​
Makala hii imejibu maswali mengi muhimu yanayohusiana na macho/jicho. Majibu yote yametoka kwa madaktari na wataalamu wa ULY CLINIC katika kitengo cha macho.
​
Bonyeza mada ili kwenda kwenye jibu lake
​
-
Kipele ndani ya jicho
-
Uvimbe kwenye jicho
​
Dalili za kuumwa macho
Karibia kila mtu ameshawahi kupata maumivu ya jicho katika maisha yake, wakati mwingine unaweza kumwangalia mgonjwa mwenye maumivu ya jicho nawewe unaanza kujihisi kama vile unamaumivu, hii ni kawaida, na husemekena kitaalamu kuwa baadhi ya madhaifu ya macho huweza kuambukizwa kwa kuangalia mtu mwenye tatizo kama ilivyo kupata hamu ya kukojoa na kupiga miayo mara unapoona mtu amefanya kitendo kimojawapo.
​
Jibu la swali letu la kuhusu dalili za maumivu ya macho;
​
Maumivu ya macho yanaweza kuambatana na dalili zifuatazo;
​
-
Uono hafifu
-
Macho kujawa na tongotongo unapoamka asubuhi
-
Macho kuwa mekundu au pinki
-
Kuhisi kuna kitu kimeingia machoni(kuhisi mchangamachoni
-
Kuumizwana mwanga
-
Maumivu ya kichwa
-
Macho kutoa machozi
-
Kutokwa na uchafu machoni
​
Maumivu ya macho pia huweza kuanzia katika sehemu yoyote ya jicho kama vile kwenye;
-
Konea
-
Sklera
-
Konjaktiva
-
Irisi
-
Misuli nje ya jicho
-
Mshipa wa fahamu
-
Nyumba ya jicho au obiti
-
Kope
-
Mishipa ya fahamu
​
Visababishi vya maumivu ya macho
​
Magonjwa au madhaifu kwenye macho yanayoweza kuleta maumivu ya jicho ni;
​
-
Ugonjwa wa blefabaitizi
-
Konjaktivaitizi
-
Michubuko ya konea
-
Maambukizi kwenye konea
-
Kitu kigeni kuingia kwenye macho
-
Glaukoma(presha ndani ya jicho)
-
Airaitizi
-
Nyuraitizi ya optiki
-
Sinusaitizi
-
Kipele kwenye jicho/chalazion
​
​
​
Dawa ya aleji ya macho
​
Aleji kwenye macho husababishwa na kuamshwa kwa kinga ya mwili dhidi ya wageni wanaojaribu kuingia kwenye macho. Wageni hawa wanaweza kuwa;
​
-
Uchafu kwenye mazingira mfano poleni za maua majani na miti,
-
Vumbi ndani ya nyumba, vumbi la mifugo na wadudu ndnai ya nyumba
-
Matumizi ya mafuta, makeup na pafyumu aina fulani
-
Aleji na lensi za kuvaa machoni
​
Dalili ya macho yenye aleji
​
Mtu mwenye aleji ya macho huanza kuonesha dalili mara tu mgeni anapoingia kwenye macho au baada ya siku mbili tatu kupita, dalili hizo huwa ni;
​
-
Macho kuonekana na rangi nyekundu au kusumbua
-
Kuwashwa
-
Kutokwa na machozi
-
Kuvimba kwa kope za macho
-
Hisia za Maumivu au kuungua kwa macho
-
Kuumizwa na mwanga
​​
Dawa za aleji ya macho
​
Ili kutibu aleji ya macho unawez akutumia dawa hizi mara baada ya kupata uchunguzi kutoka kwa daktari wako. Usitumie dawa bila ushauri kutoka kwa daktari aliyesajiliwa kutibu magonjwa kwa binadamu. Kumbuka kwenye baadhi ya nchi kila mtu anajiita daktari, kwa tanzania unaweza kubonyeza hapa kutafuta jina la daktari kama amesajiliwa na anaruhusiwa kutoa dawa na balaza na daktari wa Tanzania.
​
-
Dawa za vidonge vya antihistamine (mfano cetrizine, diphenyhydramine, fexofenadrine, loratadine
-
Dawa ya kuangushia machoni jamii ya antihistamine (mfano cetrizine, azelastine, emedastine, levocabastine na olopatadine
-
Cromolyn
-
Pemirolast
-
Lodoxamine
-
Necondromil
​
Dawa hizo hapo juu sikuzote huchanganywa na dawa zingine ambazo husaidia kusinyaza mishipa ya damu iliyovimba na kuondoa majimaji ya uvimbe kwenye macho, usitumie dawa hizi zaidi ya siku tatu kwa sababu zinaweza kukupelekea kupata macho mekundu, usitumie pia kama una ugonjwa wa glaukoma
​
​
Dawa za macho
​
Dawa za kuweza kutibu matatizo mbalimbali ya macho hutoka katika makundi mbalimbali, dawa zilizoorodheshwa hapa chini hutibu na kupunguza dalili mbalimbali zinazohusiana na macho kulingana na kisababishi.
​
-
Glaukoma- Acetazolamide
-
Macho makavu- Acetylcysteine​
-
Maambukizi ya virusi kwenye macho- Mafuta ya Aciclovir
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Antazoline and xylometazoline
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Apraclonidine
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Atropine
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Azelastine
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Azithromycin
-
Dawa ya matone na kupaka kwenye macho aina ya Betamethasone
-
Glaukoma- Betaxolol
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Bimatoprost
-
Glaukoma- Brimonidine
-
Glaukoma- Brinzolamide
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Bromfenac
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Carbomer
-
Blephagel
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Clinitas
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Carmellos
-
Glaukoma- Carteolol
-
Maambukizi ya bakteria kwenye macho- Chloramphenicol
-
Maambukizi ya bakteria kwenye macho- Ciprofloxacin
-
Cyclopentolate
-
Aleji kwenye macho- Dexamethasone
-
Mumivu ya macho- Diclofenac
-
Glaukoma- Dorzolamide
-
Homa ya hay- Emedastine
-
Homa ya hay- Epinastine
-
Mafuta ya macho- kwa macho makavu
-
Michomo kweney macho- Fluorometholone
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Flurbiprofen
-
Dawa ya matone kwenye macho aina ya Fusidic acid
-
Dawa ya maji kutibu maambukizi ya virusi kweney macho- ya Ganciclovir
-
Dawa yakutibu maambukizi ya bakteria -Gentamicin eye drops
-
Homatropine
-
Dawa ya maji aina ya- Hypromellose
-
Dawa yamaji aina ya Ketorolac
-
Dawa yamaji aina ya Ketotifen
-
Dawa yamaji aina ya Latanoprost
-
Dawa yamaji aina ya Levobunolol
-
Dawa ya kutibu maambukizi ya bakteria aina ya- Levofloxacin
-
Dawa ya maji aina ya Lodoxamide
-
Dawa ya maji aina ya Loteprednol – hutibu michomo ya macho
-
Dawa ya maji aina ya Moxifloxacin
-
Dawa ya maji aina ya Nedocromil
-
Dawa ya maji aina ya Nepafenac
-
Dawa ya maji aina ya Ofloxacin
-
Homa ya hay- Olopatadine
-
Glaucoma ya ghafla- Pilocarpine
-
Dawa ya vidonge ya Pilocarpine
-
Polyvinyl alcohol
-
Dawa kwa ajili ya aleji- Prednisolone
-
Dawa kwa ajili ya aleji- Rimexolone
-
Sodium cromoglicate
-
Macho makavu-Sodium hyaluronate
-
Macho makavu – mafuta ya Soybean
-
Tafluprost
-
Glaucoma- Timolol
-
Mambukizi kwenye macho- Tobramycin
-
Dawa ya maji- Travoprost
-
Dawa yamaji- Tropicamide
-
na zingine
Macho mekundu
Macho mekundu ni hali inayojitokeza sana, huleta mwonekano wa macho kuwa na rangi nyekundu katika sehemu ya jicho inayoitwa konjunctiva ambayo kwa kawaida huwa na rangi nyeupe. Hali ya wekundu hutokea kutokana na kupanuka kwa mishipa ya damu katika macho, utanuka huku husababishwa na hali au maambukizi mbalimbali.
Jicho jekundu linaweza kuambatana na maumivu au la. Endapo litaambatana na maumivu ni vema kumuona daktari kwa vipimo na uchunguzi. Hata hivyo jicho jekundu huweza kuathiri jicho moja au yote na mara nyingi hutokea endapo mtu akikaa kwenye mwanga mdogo ,kukosa usingizi wa kutosha na matumizi ya pombe kupita kiasi.
​
Soma zaidi kuhusu mada hii kwa kubonyeza hapa
Dawa ya macho mekundu
​
Dawa za kutibu/kupunguza dalili za macho mekundu hutegemea kisababishi, baadhi ya dawa zimeorodheshwa hapa chini, kumbuka dawa inayotibu kisababishi ni nzuri zaidi kuliko kutumia dawa za kupunguza dalili tu. Visababishi vya macho mekundu vinaweza kuwa kama glaukoma, maambukizi ya bakteria kwenye macho, aleji ya macho.
​
-
Naphazoline,.
-
Tetrahydrozoline,
-
Mafuta ya kulainisha macho
-
Na zingine
​
​Dawa zinazoweza kutibu baadhi ya visababishi ni kama vile
​
-
Endapo sababu ni glaukoma- tumia dawa za glaukoma
-
Endapo sababu ni maambukizi ya bakteria- tumia dawa za macho za antibakteria kama ofloxacine, gentamycine n.k
-
Endapo sababu ni Maambukizi ya vrusi- Tumia dawa za kutibu maambukizi ya virusi mfano aciclovir,
​
​
Kipele kwenye kope za macho
​
Kipele vya kope za macho hutokana na kuziba kwa mirija inayopitisha mafuta. Kope za macho zimetengenezwa na ngozi pamoja na tezi zinazozalisha mafuta ili kufanya ngozi hiyo isikauke. Mirija hii inapoziba husababisha mafuta kushindwa kutoka na hivyo kuleta maambukizi ya bakteria kwenye mrija hiyo iliyoziba hatimaye uvimbe kuongezeka na kuambatana na dalili mbalimbali kama zilivyoorodheshwa katika Makala hii. VIpele hivi hupendelea kutokea karibu na kona ya macho
​
​
Majina mengine yanayofanana na mada hii ni, vipele kwenye mipaka ya kope ya macho, kipele kwenye kope za macho. Stye, chalazion, vipele ndani ya kope za macho
​
Soma zaidi makala hii kwa kubofya hapa