top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

 

Je nini husababisha maumivu ya macho?


Hili ni swali  mtu anaweza kujiuliza kuhusu kisababishi cha maumivu ya macho na majibu huweza kuwa mengi.

 

Maumivu ya jicho ni ile hali inayotokea endapo kuna tatizo katika kuta za nje au ndani ya jicho. Kuwa na maumivu makali ya jicho huweza kumaanisha uwepo wa tatizo kubwa kwenye jicho linaloweza kupelekea kupoteza uono hivyo kuhitaji tiba ya haraka.

 

Maumivu ya jicho huelezewa kama hali ya jicho kuwasha, kuungua, au ya kuchoma choma. Mara nyingi maumivu ya jicho hutokana na kuingia kwa kitu kigeni kwenye macho ambacho husabaisha michomo (inflammation). Inflammation husababishwa na kuamka kwa chembe hai za mwili ili kupambana na kitu kigeni au jeraha kisha kuondoa hiyo hali. Matokeo ya inflammation ni kuzalishwa kwa kemikali zinazosababisha uhisi maumivu, kuvimba na kubadilika kwa hali ya jicho ikiwa pamoja na kuwa na rangi nyekundu, kwa pamoja inaitwa . Maumivu yanayotokea ndani ya jicho huwa na sifa za kuchoma au kuuma.

 

Sababu zinazoweza kusababisha maumivu ya jicho huwa pamoja;

​

  • Aleji/Mzio na kitu fulani

  • Michomo ya kwenye kope (kutokana na shambulio la kinga za mwili)

  • Kuziba kwa mirija ya machozi

  • Kuota kwa kifuko cha maji kwenye macho

  • Vipele ndani ya kope

  • Maumivu ya kichwa

  • Matumizi ya lensi za kuvaa machoni

  • Mikwaruzo kwenye kuta ya konea

  • Macho makavu

  • Kitu kigeni kwenye macho

  • Ugonjwa wa glaukoma

  • Majera, au kujigonga kwenye macho au kuungua

  • Michomo kwenye sehemu ya jicho yenye rangi nyeupe

  • Michomo kwenye konea

  • Michomo kwenye sehemu nyekundu ya konea

  • Michomo ya mshipa wa fahamu wa optic

  • Michomo kwenye kuta ya konjuctiva

  • Michomo kwenye ukuta wa katikati ya macho

  • Uvimbe mwekundu unaouma iliyo karibu na kingo za kope ya jicho

  • Tabia ya kugeuza kope kwa ndani au nje kwa nje

 

Unasumbuliwa na jicho?  ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua haua yoyote inayohusu afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na Tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' chini ya tovuti hii.

​

Soma zaidi kuhusu dalili zingine za macho kwa kubofya hapa

​

Imeboreshwa, 31.12.2020

​

Rejea za mada hii

​

  1. Merck Manual Professional Version. Eye pain. https://www.merckmanuals.com/professional/eye-disorders/symptoms-of-ophthalmologic-disorders/eye-pain. Imechukuliwa 30.12.2020

  2. Jacobs DS. Overview of the red eye. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 30.12.2020

  3. Ferri FF. Eye pain. In: Ferri's Clinical Advisor 2019. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 30.12.2020

  4. Pain in eye. American Academy of Ophthalmology. https://www.aao.org/eye-health/symptoms/pain-in-eye-3. Imechukuliwa 30.12.2020

  5. American Academy of Ophthalmology. Dry eye. https://www.aao.org/eye-health/diseases/what-is-dry-eye. Imechukuliwa 30.12.2020

  6. mayo clinic. Eye pain. https://www.mayoclinic.org/symptoms/eye-pain/basics/definition/sym-20050744. Imechukuliwa 30.12.2020

bottom of page