Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
8 Machi 2021, 17:00:06
Abacavir na ujauzito
Abacavir ni dawa ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI iliyo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NRTI. Dawa hii hutumika kutibu maambukizi ya HIV1. Dawa zingine zilizo kundi moja na abacavir ni didanosine, lamivudine, stavudine, zalcitabine, na zidovudine.
Ushauri wa matumizi kwa mama mjamzito
Inapatana na ujauzito kama faida kwa mama ni kubwa kuliko hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni
Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni, ina maana gani?
Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, lakini faida ni kubwa zaidi zikitumiwa na mama kuliko madhara yanayofahamika au kutofahamika kuwa yanaweza kutokea kwa kijusi-kichanganya tumboni. Kwa mama dawa zinazidi madhara yanayofahammika. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Haipatani na unyoyenyeshaji
Haipatani na unyoyenyeshaji, ina maana gani?
Kunawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha. Hata hivyo mkusanyiko wa taarifa zinaonyesha kuwa dawa huweza kuwa sumu kali kwa kichanga, au haishauriwi kunyonyesha endapo dawa itahitajika kutumika kwa mama mwenye anayehitajika kutumia dawa hii. Mama anatakiwa asinyonyeshe anapotumia dawa hii au akiwa na ugonjwa unaotakiwa kutumia dawa hii.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023, 17:21:47
Rejea za mada hii
ULY CLINIC