top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

8 Machi 2021 17:00:06

Abatacept na ujauzito

Abatacept na ujauzito

Abataceptni dawa aina ya fusion protein, inayofanya kazi ya kuzuia seli za ulinzi zenye jina la T-lymphocyte kuamshwa ili kufanya kazi, kwa kufanya hivi huzuia uzalishaji wa seli hizi za ulinzi na kuzuia uzalishaji wa kemikali zacytokine na tumor necrosis factor-α, interferon-γ, na interleukin-2 zinazoamsha maumivu, uvimbe na homa kwa wagonjwa wenye baridi yabisi. Dawa hii hutumika yenyewe au na zingine kutibu dalili za wastani au kali kwa wagonjwa walioshindikana kwa dawa zingine.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna taarifa za binadamu- Inaweza kuwa sumu

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

ULY CLINIC

bottom of page