Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
17 Machi 2021 19:53:09
Clotrimazole na ujauzito
Ufyonzwaji wa clotrimazole ni mdogo sana kwa mtu anayeweka kidonge ukeni au kupaka kwneye ngozi. Tafiti tatu kubwa zilizofanyika zimeonyesha kuwa, hakuna uhusiano wa matumizi ya dawa hii na kusababisha magonjwa ya madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii.
Hata hivyo tafiti moja imeonyesha uhusiano mkubwa wa ongezeko la mimba kutoka kwa watumiaji wa dawa hii kutibu fangasi ukeni kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito.
Kutokana na tafiti hii, ni vema kuepuka kutibu ugonjwa wafangasi ukeni au kupaka sehemu kubwa ya mwili dawa hii mpaka pale kutakapokuwa na taarifa nyingi zaidi zinazoweza thibitisha mahusiano haya.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Inapatana na ujauzito
Inapatana na ujauzito ina maana gani?
Uzoefu wa matumizi kwa binadamu kuhusu dawa hii au dawa zingine zilizo kundi moja au zenye kufanya kazi kwa utaratibu unaofanana, zinatosha kuonyesha kuwa, madhara kwa kichanga tumboni ni madogo sana au hakuna kabisa. Tafiti za uzazi kwa wanyama hazina uhalisia kwa binadamu.
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Inapatana na unyonyeshaji
Inapatana na unyonyeshaji ina maana gani?
Kiasi kidogo cha dawa hii kinawezekana kuingia kwenye maziwa ya mama, kiasi hiki hakina mashiko ya kusababisha sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii haitarajiwi kusababisha madhara kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023 17:21:36
Rejea za mada hii
1. Tan CG, et al. A comparative trial of six-day therapy with clotrimazole and nystatin in pregnant patients with vaginal candidiasis. Postgrad Med 1974;50(Suppl 1):102–5.
2. Frerich W, Gad A. The frequency of Candida infections in pregnancy and their treatment with clotrimazole. Curr Med Res Opin 1977;4:640–4.
3. Haram K, Digranes A. Vulvovaginal candidiasis in pregnancy treated with clotrimazole. Acta Obstet Gynecol Scand 1978;57:453–5.
4. Svendsen E, et al. Comparative evaluation of miconazole, clotrimazole and nystatin in the treatment of candidal vulvo-vaginitis. Curr Ther Res 1978;23:666–72.
5. Product information. Lotrimin. Schering, 2000.
6. Rosa FW, et al. Pregnancy outcomes after first-trimester vaginitis drug therapy. Obstet Gynecol 1987;69:751–5.
7. Czeizel AE, et al. No teratogenic effect after clotrimazole therapy during pregnancy. Epidemiology 1999;10:437–40.
8. Kragie L, et al. Assessing pregnancy risks of azole antifungals using a high throughput aromatase inhibition assay. Endocr Res 2002;28:129–40.
9. Harada N. Genetic analysis of human placental aromatase deficiency. J Steroid Biochem Mol Bi ol 1993;44:331–40.