top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

19 Machi 2021, 18:44:11

Isoniazid na ujauzito

Isoniazid na ujauzito

Isoniazid haionekani kuwa kundi la dawa zinazofahamika kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii wakati wa ujauzito. Inashauriwa kuendelea kutumia dawa hii endapo imechaguliwa kutumika kwa sababu hatari za TB kwa mama ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtoto kutokana na kutumia dawa hii.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni


Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni, ina maanisha nini?

Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, lakini faida ni kubwa zaidi zikitumiwa na mama kuliko madhara yanayofahamika au kutofahamika kuwa yanaweza kutokea kwa kijusi-kichanganya tumboni. Kwa mama dawa zinazidi madhara yanayofahammika. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji, ina maanisha nini?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023, 17:21:36

Rejea za mada hii

bottom of page