Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
13 Machi 2021 20:01:41
Ivermectin na ujauzito
Ivermectin ilikuwa kisababishi cha ulemavu kwa kichanga kwenye tafiti za wanyama jamii tatu, lakini kwenye dozi ambayo ni sumu kwa binadamu. Hakuna taarifa za kusababisha matatizo ya kiuumbaji kwa kichanga zilizoonekana kwenye taarifa chache za matumizi wakati wa ujauzito. Mapitio ya shirika la afya duani ya mwaka 1997 kuhusu taarifa za dawa hii yalitoa uamuzi kwamba, kutokana na hatari kubwa ya mama kupata upofu wa mtoni (usubi) kutoka kwenye maambukizi ya onchocerciasis, na kukosekana kwa taarifa za maudhi kwenye ujauzito, matumizi ya ivermectin kipindi cha kwanza cha ujauzito, yanaweza kukubalika.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga
Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga, inamaanisha nini?
Kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu kutoka kwenye dawa hii au dawa zilizo kundi moja au zinazofanana namna zinavyofanya kazi yake. Ikijumuisha ujauzito miezi mitatu ya kwanza, inaonyesha kuwa, dawa hii haiwakilishi kuwa na hatari yenye mashiko ya kuwa sumu kwa kichanga tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika muda wowote ule kwenye ujauzito. Taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu zinafanya taarifa za uzazi wa wanyama kutokuwa na mashiko
Hakuna (zinapatikana chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (zinapatikana chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji, inamaanisha nini?
Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.
Kanamycin na ujauzito
Dawa hiii imeripotiwa kuwa sumu kwenye masikio, hata hivyo hakuna ripoti ya kusababisha madhaifu mengine ya kiumbaji ya maungo mbalimbali ya mwili kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Taarifa za binadamu (wanyama) zinaonyesha hatari ya kupata madhara
Taarifa za binadamu (wanyama) zinaonyesha hatari ya kupata madhara ina maanisha nini?
Taarifa za matumizi ya dawa hii au zile zilizo kundi moja na hii au zile zinazofanana namna zinavyofanya kazi na hii kwa binadamu na wanyama wajawazito , imeonekana kuwa sumu kwenye uumbaji wa kichanga tumboni kwa na kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo cha kichanga au kijusi tumboni katika kipindi chote cha ujauzito. Hata hivyo hatari inaweza kuvumiliwa endpo shida ya mama inahitaji dawa hii.
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji ina maanisha nini?
Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023 17:21:36
Rejea za mada hi
1. de Silva N, et al. . Anthelmintics. A comparative review of their clinical pharmacology.Drugs 1997;53:769–88.
2. Product information. Stromectol. Merck, 2002.
3. Pacque M, et al. Pregnancy outcome after inadvertent ivermectin treatment during community-based distribution. Lancet 1990;336:1486–9.
4. Chippaux JP, et al. Absence of any adverse effect of inadvertent ivermectin treatment during pregnancy. Tran R Soc Trop Med Hyg 1993;87:318.
5. Ogbuokiri JE, et al. Ivermectin levels in human breastmilk. Eur J Clin Pharmacol 1993;45:389–90.
6. Committee on Drugs, American Academy of Pediatrics. The transfer of drugs and other chemicals into human milk. Pediatrics 2001;108:776–89.