Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
17 Machi 2021 19:13:57
Paromomycin na ujauzito
Paromomycin ni dawa jamii ya aminoglycoside inayotumika kutibu ugonjwa wat umbo wa amebiasis. Hakuna ripoti iliyoandikwa kuzungumzia mahusiano ya dawa hii na madhaifu ya kiuumbaji. Dawa hii hufyonzwa kidogo sana tumboni na inayoingia kwenye damu hutolewa yote kwa asilimia 100 kwenye haja kubwa bila kufanyiwa umetaboli, hivyo hakuna kiasi cha dawa au kuna kiasi kidogo kabisa huweza kuingia kwa kijusi tumboni.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Hakuna taarifa(taarifa ni chache) ya kuwepo madhara kwa binadamu- inaweza kupatana na ujauzito
Hakuna taarifa(taarifa ni chache) ya kuwepo madhara kwa binadamu- inaweza kupatana na ujauzito, ina maana gani?
Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, hata hivyo sifa ya ufanyaji kazi wa dawa inaonyesha kutokuwa na hatari yenye mashiko kusababisha madhara kwa kichanga aliye tumboni. Kwa mfano dawa zingine kwenye kundi moja au zenye kufanana ufanyaji kazi zinapatana na ujauzito au kiwango cha dozi ya dawa kwenye damu hakina mashiko kusababisha madhara. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshajiina maana gani?
Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023 17:21:36
Rejea za mada hii
1. Kreutner AK, Del Bene VE, Amstey MS. Giardiasis in pregnancy. Am J Obstet Gynecol 1981;140:895–901.
2. D’Alauro F, Lee RV, Pao-In K, Khairallah M. Intestinal parasites and pregnancy. Obstet Gynecol 1985;66:639–43.