Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
19 Machi 2021 19:28:53
Tenofovir na ujauzito
Ingawa taarifa za wanyama zinaonyesha hatari kwenye ujauzito kwa kupunguza ukuaji wa kichanga, taarifa hazijitoshelezi kutoa ushauri kuhusu dawa kusababisha madhaifu ya kiuumbaji. Taarifa za uzoefu wa matumizi ya dawa hii kutoka kwa biandamu wajawazito ni chache na hazitoshi kutoa hitimisho la hali yake kwenye ujauzito. Endapo itapendekezwa kutumika, haitakiwi kusimamishwa kwa sababu ya ujauzito hata hivyo ni uchunguzi wa figo unatakiwa kufanyika kuangalia kama inaleta madhara kwa sababu dawa hii huwa sumu kwenye figo.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni
Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni, ina maana gani?
Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, lakini faida ni kubwa zaidi zikitumiwa na mama kuliko madhara yanayofahamika au kutofahamika kuwa yanaweza kutokea kwa kijusi-kichanganya tumboni. Kwa mama dawa zinazidi madhara yanayofahammika. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano.
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Haipatani na unyoyenyeshaji
Haipatani na unyoyenyeshaji, ina maana gani?
Kunawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha. Hata hivyo mkusanyiko wa taarifa zinaonyesha kuwa dawa huweza kuwa sumu kali kwa kichanga, au haishauriwi kunyonyesha endapo dawa itahitajika kutumika kwa mama mwenye anayehitajika kutumia dawa hii. Mama anatakiwa asinyonyeshe anapotumia dawa hii au akiwa na ugonjwa unaotakiwa kutumia dawa hii.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023 17:21:36
Rejea za mada hii
1. George K. SIBERRY, MD, MPH , et al. Safety of Tenofovir Use During Pregnancy: Early Growth Outcomes in HIV-Exposed Uninfected Infants https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3476702/Imechukuliwa 19.03.2021
2. Table 10. Antiretroviral Drug Use in Pregnant Women with HIV: Pharmacokinetic and Toxicity Data in Human Pregnancy and Recommendations for Use in Pregnancy. Inapatikana https://clinicalinfo.hiv.gov/en/table/table-8-antiretroviral-drug-use-pregnant-women-hiv-infection-pharmacokinetic-and-toxicity.Imechukuliwa 19.03.2021
3. Tarantal AFet al. Administration of 9-[2-(R)- (phosphonomethoxy)propyl]adenine (PMPA) to gravid and infant rhesus macaques (Macaca mulatta): safety and efficacy studies. J Acquir Immune Defic Syndr Hum Retroviral 1999;20:323–33.
4. Tarantal AF, et al. Fetal and maternal outcome after administration of tenofovir to gravid rhesus monkeys (Macaca mulatta). J Acquir Immune Defic Syndrome 2002;29:207–20.
5. Carpenter CCJ, et al. Antiretroviral therapy for HIV infection in 1996. JAMA 1996;276:146–54.
6. Minkoff H, Augenbraun M. Antiretroviral therapy for pregnant women. Am J Obstet Gynecol 1997;176:478–89.
7. Minkoff H. Human immunodeficiency virus infection in pregnancy. Obstet Gynecol 2003;101:797–810.
8. Brown ZA, Watts DH. Antiviral therapy in pregnancy. Clin Obstet Gynecol 1990;33:276–89.
9. De Martino M, et al. HIV-1 transmission through breast-milk: appraisal of risk according to duration of feeding. AIDS 1992;6:991–7.
10. Van de Perre P. Postnatal transmission of human immunodeficiency virus type 1: the breast-feeding dilemma. Am J Obstet Gynecol 1995;173:483–7.