USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA KIPINDI CHA UJAUZITO NA KUNYONYESHA

Cephalexin kwenye ujauzito
Cephalexin antibayotiki kundi la cephalosporin, dawa hii hutumiwa kwa kunywa. Tafiti za panya zimeonyesha kuwa cephalexin haina madhara kwa kijusi tumboni kwenye dozi ya miligramu 500 kwa kilo, dozi inayoweza pelekea kuingilia uumbaji wa kijusi cha panya akiwa tumboni.
Ingawa dawa hii imeonekana kutosababisha madhara ya kimaumbile kwa mtoto, tafiti moja imeleta mkang’anyiko kwa kuonyesha kuwa dawa cephalexin inahusiana na madhaifu ya kiuumbaji kwa kijusi ambayo ni madhaifu ya moyo, tatizo la mgongo wazi, kuzaliwa na vidole vingi, kupungua kwa mikono au miguu, na haipospadiasisi.
Madhara haya kwenye tafiti yamelezewa kuhusiana na matatizo waliyokuwa nayo wazazi, matumizi ya dawa zingine au mambo mengine.
Tafiti nyingine pia imeonyesha kuhusiana na madhaifu ya moyo na mdomo sungura kwa watoto wa mama waliotumia dawa hii kwenye ujauzito.
Kiasi kidogo huingia kwenye maziwa ya mama na humpata mtoto na kuleta madhara ya kubadilisha bakteria rafiki kwenye mfumo wa tumbo la mtoto, kutoa majibu ya kuotesha bakteria yasiyo sahihi endapo mtoto ana homa na madhara ya moja kwa moja kwa mtoto. Tafiti moja inaonyesha kuwa mama alipotumia dawa hii pamoja na probenecid ilihusiaa na madhara kwa mtoto. Hata hivyo wataaluma wameweka dawa hii kuwa salama kutumika kwa mama aonyonyesha.
Ingawa baadhi ya tafiti zimeonyesha kuhusiana na madhaifu ya kiuumbaji kwa mtoto, kwa ujumla imeonekana kuwa ni salama kutumika wakati wa ujauzito.