top of page

Magonjwa na saratani mbalimbali

Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Ugonjwa amibiasis

Ugonjwa amibiasis

Ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya kimelea Entamoeba histolytica. Ugonjwa huu huweza kutokea bila dalili, au kusababisha dalili kama kuhara damu, maumivu ya tumbo, na katika hali mbaya zaidi, vidonda vya utumbo na majipu kwenye ini.

Saratani ya Uke

Saratani ya Uke

Saratani ya uke ni aina nadra ya saratani inayotokea kwenye tishu za uke. Inapoanza, inaweza kuwa na dalili zisizo za wazi na kipekee, lakini utambuzi wa mapema ni muhimu kwa matibabu yenye mafanikio.

Shinikizo la chini la damu

Shinikizo la chini la damu

Kuwa na shinikizo la chini la damu huweza kuonekana ni hali nzuri kwa baadhi ya watu, hata hivyo huweza sababisha hali ya kupatwa na kizunguzungu na kuzimia na ikitokea limeshukwa kupita kawaida huweza pelekea mtu kupoteza maisha.

Vibarango na Mapunye

Vibarango na Mapunye

Hutokana na maabukizi kwenye ngozi yanayosababishwa na fangasi Trichophyton na Microsporum ambao hupenda kudhuru mashina ya vinyweleo licha ya kuweza kusambaa kwenye kope ya jicho.

bottom of page