top of page

Mwandishi:

Mhhariri

Dkt. Benjamin L, MD

Mahariri:

Jumanne, 28 Desemba 2021

Kisonono

Kisonono

Kisosono ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aina ya bakteria anayeitwa Neisseian gonorrhoeae, ugonjwa huu unaoambukizwa kwa njia ya kujamiiana au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa hutibika endapo mtu atapata matibabu sahihi.


Shirika la centre for didease control (CDC) linashauri kwamba watu wote wenye wanaopata ugonjwa huu ni lazima watibiwe maambukizi ya chlamydia trachomatis kwa sababu huweza kutokea pamoja na Kisonono

Ugonjwa huu unatokea sana kwa vijana walio na umri chini ya miaka 25 kwa sababu ya kuwa na wapenzi wengi, kukosa fursa za huduma na elimu ya kiafya na kupungua matumizi ya utumiaji wa kondomu kama njia ya uzazi wa mpango.


Baadhi ya wanawake huwa hawaonyeshi dalili za ugonjwa huu lakini kwa wanaume ni nadra sana kutoonyesha dalili na hutokea kwa uwiano wa 1:1 kati ya wanaume na wanawake. Matatizo makubwa yatokanayo na ugonjwa huu hutokea kwa wanawake. Kwa vile ugonjwa huu huathiri maeneo ya shingo ya kizazi, kama usipotibiwa matokeo yake vimelea hawa hupanda katika mfuko wa kizazi na kusababisha maambukizi ya mfuko wa kizazi-pelvic inflamatory disease(PID) ambai unaweza kusababisha ugumba, kutunga kwa mimba nnje ya mfuko wa uzazi na maumivu sugu ya nyonga. Maambukizi kwa watoto wadogo humaanisha mtoto amefanyiwa kitendo cha unyama

Vimelea wa ugonjwa wanapoingia mwilini mwa binadamu huweza kukaa siku 2-7 kujizalia mwilini na mtu anaonyesha dalili siku 10 toka alipo ambukizwa. Mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa huu lazima aulizwe mambo ya fuatayo

  • Historia ya magonjwa ya zinaa kabla ya tatizo hili

  • Historia ya kutibiwa magonjwa ya zinaa

  • Historia ya mwezi kutibiwa magojwa ya zinaa

  • aina yanjia za uzazi wa mpango unazotumia

  • na historia ya kufanyiwa kitendo cha ngono pasipo ridhaa

Mambo haya huweza kusaidia katika matibabu ya mgonjwa

Dalili za ugonjwa huu ni zipi?

​

Dalili wanazoonyesha wanaume ni;


  • kuhisi kuungua wakati wa kukojoa

  • uchafu mweupe, wanjano au wakijani ukitoka kwenye uume. kama hautoki, uume ikikamuliwa basi uchafu huu huweza kutoka.

  • Kuvimba kwa korodani(dalili hii huwa haitokei sana)

  • Wakati mwingine kuziba kwa mrija wa urethra hivo kushindwa kukojoa lakini hili ni kwa nadra sana

Wanawake maranyingi huwa hawana dalili na hata kama wana dalili maranyingi huwa za kujizuia na zinaweza zikadhaniwa kuwa anamaambukizi ya kibofu cha mkojo au uke, wanawake wenye kisonono huweza kupata madhara ya ugonjwa huu kama wasipotibiwa hata kama hawana dalili, dalili zikiwepo wanaweza kuonyesha kati ya hizi zifuatazo;


  • Kuhisi maumivu na kuungua wakati wa kukojoa

  • Kutokwa/kuongezeka kutokwa na uchafu ukeni

  • Kutokwa na damu ukeni kabla ya mzunguko wa hedhi kufika

  • Maumivu ya chini ya mgongo

  • Au maumivu ya juu kulia ya tumbo kama vimelea wamegusa Ini

  • Homa

​

Maambukizi ya kisonono kwenye njia ya haja kubwa yanaweza kuonyesha dalili zifuatazo;


  • Kutokwa uchafu kama mlenda mweupe

  • Kuwashwa

  • Kutokwa damu

  • Kupata maumivu ya tumbo

  • Kuwa mkavu

Kwa watu wenye maambukizi ya mdomoni kutokana nakufanya ngono kwa njia ya mdomo huwa na dalili zifuatazo;


  • maambukizi ya koo(pharyngitis) yanayosababisha koo kuuma

  • kutokwa namlenda lenda mweupe

Dalili kwa watoto wenye maambukizi haya ni;


  • Kutokwa na mlendalenda mweupe katika macho yote mawili kama mtoto ni mdogo au jicho moja kama mtoto ni mkubwa

  • Anaweza kuwa na homa kama ugonjwa umesambaa kwenye damu

Ugonjwa ukisambaa unaweza kwenda katika mfumo wa fahamu na kusabisha uti wa mgongo(meningitis), maungio ya mwili na kusababisha maumivu ya maungio, maumivu ya misuli au kufanyika kwa usaa kwenye misuli , ngozi-kupata mabaka makubwa sehemu ya nyayo za miguu, viganja vya mikono , mabaka haya hayatokei katika uso kichwa na mdomo. Kwa wagonjwa walio athirika na VVU huwa na maumivu makali ya maungio(arthritis) na hata kuharibiwa kwa maungio pamoja na homa.

Vipimo vya ugonjwa huu ni vipi?

Mara utakapofika hospitali dakitari atachukua historia yako na kisha ataweza kuingiza kijiti kilicho na pamba na kuchukua majimaji kwenye shingio ya kizazi, koo, urethra, mkunduni (inategemea ikitegemea dalili zako) kisha kwenda kuotesha vimelea. Hii ndio njia nzuri ya kufanya kipimo hiki kwani huonyesha kimelea gani ameathiri sehemu hizo na anatibika na dawa gani. Kwa vile kipimo hiki huchukua mda basi dakitari ataamua kukutibu kwa kutumia dawa kwa sababu ugonjwa unaweza kugunduliwa kutoka katika historia yako na uchunguzi wa awali wa physical examination. Kabla hujaanzishiwa dawa utapimwa ujauzito na vipo vipimo vingine vinaweza kufanyika pia kutegemea unaonyesha dalili gani.

Kumbuka:


Matibabu ya ugonjwa huu huhusisha kutibu mtu na mpenzi wake, kama umeathilika na ugonjwa huu dakitari ataomba umlete mpenzi wako ili muanzishiwe matibabu wote maana utakapotibiwa peke yako unaweza kuambukizwa tena mtakaposhiriki tendo la ndoa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

28 Desemba 2021, 20:17:21

Rejea za mada hii:

1. CDC fact sheet (detailed version). Gonorrhea. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/std/gonorrhea/stdfact-gonorrhea.htm. Imechukuliwa 28.12.2021

2. Ghanem KG. Clinical manifestations and diagnosis of Neisseria gonorrhoeae infection in adults and adolescents. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.12.2021

3. Office on Women's Health. Gonorrhea. . https://www.womenshealth.gov/a-z-topics/gonorrhea. Imechukuliwa 28.12.2021

4. Merck Manual Professional Version. Gonorrhea. https://www.merckmanuals.com/professional/infectious-diseases/sexually-transmitted-diseases-stds/gonorrhea. Imechukuliwa 28.12.2021

5. Chlamydia, gonorrhea, and nongonococcal urethritis. Mayo Clinic; 2019.
Speer ME. Gonococcal infection in the newborn. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.12.2021

bottom of page