Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Benjamin L, MD
Dkt. Peter A, MD
Jumapili, 14 Novemba 2021
Sunzua
Sunzua ni aina ya uoto utokeao kwenye ngozi laini na ngumu na husababishwa na anuai mbalimbali za kirusi human papillomavirus (HPV).
Kuna anuai zaidi ya 100 ya kirusi HPV, hata hivyo kuna anuai zinazosababisha sunzua maeneo mbalimbali kama vile anuai ya 6 na 11 husababisha sana sunzua kwenye maeneo ya siri.
Matibabu ya suzua yanaweza kuwa magumu na baadhi ya nyakati sunzua huisha zenyewe bila tiba.
Usambazaji
Maambukizi ya HPV yanaweza kutokea kwa kushika sunzua au kwa njia ya kujamiana kama wapo maeneo ya siri. Matukio yoyote yanayoongeza hatari ya kuharibu ukuta wa ngozi huongeza hatari ya kupata sunzua.
Sunzua inaweza kuwa saratani?
Sunzua inaweza kubadilika kuwa saratani kwa baadhi ya watu wenye vihatarishi kama vile wale wenye upungufu wa kinga mwilini na wale wenye maambukizi ya kirusi HPV anuani ya 5, 8, 20 na 47.
Aina za sunzua
Kuna aina mbalimbali za sunzua ambazo zimegawanywa kulingana na sehemu ya mwili iliyoathirika na kirusi
kilichosababisha. Aina hizo ni;
Sunzua ya kawaida- Husababishwa sana na anuai 2 na 3 ya kirusi HPV ikifuatiwa na 1, 3, 27, 29, na 57
Sunzua bapa:- Husababishwa na anuai ya 3, 10 na 28 ya kirusi HPV
Sunzua ya shini ya ngozi ya viganja na kanyagio:- Husabaishwa sana na anuai ya 1 ya kirusi HPV ikifuatiwa na anuai ya 2, 3, 4, 27, na 57 ya kirusi HPV
Sunzua ya kifuko cha maji:- Husababishwa na anuai ya 60 ya kirusi HPV
Sunzua inayoathiri epithelia:- Husababiswha na anuai ya 13 na 32 ya kirusi HPV
Sunzua ya Bucha:- Husababiswha na anuai ya 7 ya kirusi cha HPV
Dalili
Mara nyingi sunzua huwa haina dalili yoyote ile, hata hivyo huweza kuhariu mwonekano wa sehemu ilipoota na kwa wagonjwa wachache inaweza kusababisha maumivu.
Sunzua inayoota kwenye kanyagio huambatana na maumivu makali kwa sababu ya mgandamizo unaotokea na wakati mwngine inaweza kutoa damu na kuathiri mjongeo wa mtu.
Sunzua ya kawaida huwa kama kipele kidogo kisichoeleweka kontua na chenye urefu kuanzia sentimita 1 nakadharika.
Sunzua za kawaida mara nyingi huoekana mikononi au miguuni
Sunzua za kawaida zinaoonekana maeneo ya kuzunguka midomo na kope huweza kuwa ndefu na nyembamba.
Sunzua kwenye kanyagio na viganja vya mikono huwa na umbo na hupatikana chini ya ngozi kiasi cha kuweza kufikiriwa kuwa ni sugu, hata hivyo sifa zake ni kuwa na maumivu kama maeneo yeye sunzua yakishikwa.
Sunzua bapa huonekana kama uoto wenye ukubwa wa milimita 1 hadi 7 na idadi yake huweza mamia.
Sunzua ya bucha huonekana kwa watu wanaojihusisha na kushika nyama na mazao ya nyama. Huwa na mwonekano wa kama uyoga bapa unaoota kwenye gome la na huwa mkubwa pia.
Sunzua ya epithelia hutokea kwenye kuta za kinywa na midomo. Huonekana kama vipele vidogo vyeupe vyenye ukubwa wa milimita 1 hadi 5 na hukaa kwenye makundi.
Sunzua ya kifuko cha maji hutokea kwenye maeneo yanayobeba uzito wa mwili kama vile kanyagio na huwa na kuta laini.
Matibabu ya sunzua
Baada ya kufahamika kwa kuchunguza wa sunzua, matibabu yake hutegemea dalili, uchaguzi wa mgonjwa na gharama. Licha ya kuwa na matibabu aina kadhaa ya sunzua, hakuna matibabu yenye ufanisi mkubwa na mara nyingi hujirudia kwa aina nyingi za matibabu yaliyopo. Unapaswa kuchagua matibabu ya gharama nafuu na yasiyokuletea maumivu.
Matibabu ya dawa
Dawa za kupaka ambazo huandikwa na daktari kama;
Salicylic acid
Retinoic acid
Podophyllin
5-fluorouracil
Interferon
Imiquimod
Cidofovir
Cryotherapy
Bleomycin
Cimetidine
Matiabu yasiyo dawa
Matibabu asili na tiba isiyo dawa ya sunzua huhisisha;
Tiba ya makovu
Hypnosis
Tiba joto
Matumizi ya tiba kutoka kwenye viini vya mimea
Matibabu ya upasuaji
Matibabu ya sunzua kwa upasuaji huhusisha;
Kukausha sunzua kwa barafu
Kukata sunzua kwa mwanga wa laser
Kukata sunzua kwa kisu cha umeme
Kukata sunzua kwa kisu
Magonjwa yanayofanana
Magonjwa yanayofanana na sunzua kiasi cha kuchanganywa nayo ni;
Molluscum contagiosum
Seborrheic keratosisi
Lichen planus
Saratani ya seli za squamous
Keratoacanthoma