Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Jumanne, 22 Juni 2021
Fangasi kwenye pumbu
Maambukizi ya fangasi kwenye kinena hufahamika kwa jina jingine la tinea kruriz ni ugonjwa unaosababishwa na kuzaliana kupita kiasi kwa fangsi waishio kwenye ngozi wenye jina Trichophyton rubrum, Epidermophyton floccosum na T. mentagrophytes.
Fangasi kwenye kinena huota kwenye maneoa kati ya mashavu ya uke na mapaja au kwenye mapaja karibia na maeneo ya siri na maeneo chini kidogo ya kibofu cha mkojo.
Fangasi hawa wanaopata mazingira mazuri ya kuzaliana zaidi, huzaliana kiasi kwamba kusababisha kuonekana kwa dalili za mwasho kwenye kinena na zingine.
Mazingira rafiki kwa fangasi wa kinena kuzaliana
Mazingira mazuri yanayofanya fangasi waishio kwenye ngozi ya kinena kuzaliana zaidi ni yale;
Yenye ujoto
Yasiyo na hewa
Yenye unyevu
Mazingira hayo huwapa fangasi fursa ya kuzaliana kupita kiasi na kwenye maeneo mengine kama kwapani na kwenye uvungu wa titi kwa mwenye titi lililolala
Dalili za maambukizi ya fangasi kwenye kinena
Dalili zifuatazo huonekana kwa wagonjwa wenye fangasi wa kinena;
Muwsasho kwenye kinena unaosababisha kujikuna na kuona raha lakini baadae hufuatiwa na maumivu makali
Maumivu kwa mbali
Kuonekana kwa magamba madogo kwenye korodani au maeneo ya kinena
Kwa wenye ngozi nyeupe, ngozi kuwa na mabaka ya rangi nyekundu na weusi hupata mabaka ya rangi ya zambarau au pinki iliyokole kabla ya kupata miinuko
Kuonekana kwa miduara iliyocholeka vizuri katika kingo, inaweza kuwa na miinuko midogo katikati yake
Kuathirika kwa upande wa kulia na kushoto ya kinena au mapaja
Vipimo vya fangasi wa kinena
Mara nyingi vipimo huwa havihitajiki kutambua fangasi wa kinena , daktari atakagua maeneo ya siri na kukuuliza historia ya tatizo na kufahamu tatizo lako. Endapo atahitaji kutofautisha au kuthibitisha tatizo hili na mengine, vipimo vitahitajika vifuatavyo vitaombwa kufanyika;
Potassium hydroxide wet mount
Matibabu ya fangasi kwenye kinena
Matibabu huhusisha matumizi ya dawa za fangasi za kupata au za kunywa ambazo utaandikiwa na daktari wako.
Baadhi ya dawa zinazoweza kutumika kutibu fangasi kwenye kinena;
Ketoconazole ( nizoral)
Itraconazole (sporanox)
Clotrimazole (mycelex)
Terbinafine (lamisil)
Ciclopirox (loprox, penlac)
Miconazole (monistat 3)
Econazole (ecoza)
Orodha ya dawa zingine imeandikwa katika Makala ya dawa za kutibu fangasi maeneo ya siri ndani ya tovuti hii ya ulyclinic
Magonjwa yanayofanana na fangasi wa kinena
Lichen simpleksi
Soriasis
Demataitiz ya mguso
Demataitiz ya Seborrheic
Erythrasma
Kinga
Oga na safisha maeneo ya kinena kila siku kisha kausha na kupaka mafuta. Usivae nguo ya ndani ukiwa na unyevu kwenye maeneo haya.
Kata nywele za maeneo ya siri ziwe fupi kuzuia kuleta ujoto, mazingira mazuri ya kuzaliana kwa fangasi
Vaa nguo ya ndani safi kila siku, usivae nguo moja zaidi ya siku moja na unapoivua usiirudie kwani fangasi hukua kwenye nguo pia zenye uvundo
Vaa nguo zinazoruhusu hewa kuingia kwenye kinena
Pima na pata tiba ya fagasi wengine wa miguu ili wasasambae kwenye maeneo ya kinena
Usitumie taulo na mtu mwingine au taulo zile zinazopatikana kwenye nyumba za wageni kuepuka kupata maambukizi ya fangasi
Usitumie taulo yako na watu wengine ili kuepuka kuwapa au kupokea maambukizi ya fangasi