top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

ULY CLINIC

Jumanne, 12 Septemba 2023

Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo

Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo

Katika makala hii tumezungumza UTI kwa kuwataja wanawake lakini makala hii inaweza kutumika kwa wanaume na watoto pia

UTI ni ugonjwa unaosumbua sana wanawake, ugonjwa huu unasababishwa na kupanda kwa vimelea vya bakiteria kutoka ukeni na kuingia kwenye mrija unaotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu yaani urethra.

Wadudu hawa wanaweza wasiishie kwenye kibofu tu bali wanaweza kukwea na kufika katika mirija inayotoa mkojo kutoka kwenye figo ijulikanayo kama ureta na hatimaye kuingia kwenye figo. Mfumo wa mkojo kwa binadamu umegawanywa katika sehemu mbili, mfumo wa chini wa mkojo ambao ni kibofu na urethra na mfumo wa juu wa mkojo ambao unaundwa na ureta na figo

 

Maambukizi ya mfumo wa chini hutokea kwa wingi kuliko ule wa mfumo wa juu, ingawa maambukizi ya mfumo wa juu yanatokea  ni kwa nadra sana na endapo maambukizi yatatokea basi  maranyingi hua yameambatana na magonjwa/hali zingine kwa mgonjwa kama ugonjwa wa kisukari, watu wanaoitumia dawa za kushusha kinga mwilini, wanaotumia dawa za kutibu Saratani(mionzi na dawa za kumeza au kuwekwa kwenye mishipa), watu waliobadilishiwa figo na magonjwa mengine sugu.

 

UTI ikitokea kwenye mfumo wa juu huleta matatizo makubwa na mwishowe kama yasipotibiwa huweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi n.k

Kutokana na anatomia ya mfumo wa mkojo wa mwanamke(maumbile asilia) mrija unaotoa mkojo kwenye kibofu huwa mfupi ukilinganisha na mrija huu kwa wanaume, hili linapelekea vimelea vya magonjwa kupanda kirahisi  kufikia kibofu cha mkojo  kisha kujizalia na kuleta dalili za ugonjwa huu wa Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo

UTI hutokeaje mara kwa mara?

 

Mkojo mara nyingi huwa ni safi na una kemikali za asidi na urea zinazoweza kuuwa vimelea vinavyojalibu kuingia kwenye mfumo wa mkojo. Pia mwili unauwezo wa kuzuia vimelea vya magonjwa kupanda kwa kupeleka kinga za mwili mara vimelea vinapojaribu kuingia kwenye mfumo huu. Endapo mtu ana mfumo wa kinga mwilini usiofanya kazi vizuri au anatomia inaruhusu kueneza kwa vimelea hivi au kama vimelea ni sugu kwenye dawa au wanasifa zinazowafanya waweze kuishi licha ya mfumo wa kinga kuwa vizuri basi mtu anapata maambukizi haya mala kwa mala.

Vimelea gani wanaosababisha UTI?

Kimelea aina ya Escherician coli (E.coli) husababisha ugonjwa huu kwa asilimia nyingi, vimelea hawa hupatikana kwenye njia ya haja kubwa kama kimelea asilia maeneo hayo na akisafilishwa kwa njia ya kutawaza kama mwanamke anapotawaza akitoka haja kubwa, akitawaza kutoka nyuma kwenda mbele huweza kupandikiza vimelea ukeni kisha  husafili kuingia kwenye mirija ya mkojo. Vimelea wengine ni kama Staphylococcus saprophyticus, Proteus species, Klebsiella species, enteroccocus faecalis, enterobactericeae na fungus

 

Baadhi ya vimelea hutokea kwenye umri fulani, wanawake wenye umri mdogo wanaambukizwa na kimelea aina ya  staphylococcus saprophyticus.

 

Vihatarishi vinavyoweza kufanya upate UTI ni vipi?


Sababu zifuatazo zinaweza kukusababisha upate UTI

  • Mara nyingi UTI huambukizwa hospitalini kwa sababu ya kuwekewa mpira wa mkojo (catheter) na kukaa muda mrefu---matumizi ya catheter yasiyo salama yanaweza kukuingizia vimelea kwenye kibofu na kusababisha UTI. Kwa hiyo ni vema kubadilishiwa catheter baada ya wiki mbili au tatu ili kuzuia kupata UTI

  • Endapo mpira wa mkojo unawekwa juu ya usawa wa mwili mkojo unahatari ya kutuama pasipo kuingia kwenye mfuko wa mkojo(cather bag)  na  kuongeza hatari ya kurudi nyuma na kuingia kwenye kibofu na kama umeambulkizwa unasababisha maambukizi kwenye kibovu

  • Pia uchunguzi wa sehemu za uke na njia ya kinyesi usio salama unaweza kusababisha usafilishaji wa vimelea hawa kutoka kwenye kinyesi kwenda kwenye mfumo wa mkojo

  • Tendo la ndoa, matumizi ya vipandikizi huweza kupandikiza vimelea hawa kwenye uke na kuleteleza ugonjwa huu

  • Wanawake wajawazito na walio na matatizo ya kuzaliwa nayo kwenye mfumo wa mkojo wanapata maambukizi ya ugonjwa huu mara kwa mara

  • Kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa figo na kisha kuwekwa kwenye dawa za kushusha kinga ya mwili unaongeza hatari ya kupata UTI mara kwa mara

  • Tatizo la mkojo kurudu nyuma kutoka kwenye kibofu kuingia kwenye figo( vesicoureteric reflux disease) husababisha UTI mara kwa mara

  • Kushuka kwa kinga ya mwili kama kwa wagonjwa wa kisukari ni kihatarishi cha kupata UTI mara kwa mara

 

Zipi ni dalili za UTI?

Dalili ya za awali za mtu mwenye UTI ni maumivu wakati wa kukojoa yanayoambatana na

 

  • Kuwa na haja ya kukojoa mara unapo banwa na mkojo na kwenda haja ndogo mara kwa mara

  • Kuhisi mkojo umejaa kwenye kibofu

  • Kujihisi na hali isiyo ya kawaia kwenye tumbo chini ya kitovu

  • Maumivu nyuma ya mgongo kwenye miishio ya ubavu na maumivu ubavuni kama ukishikwa( ingawa huonekana sana kwenye maabukizi ya mfumo wa juu wa mkojo)

  • Damu kwenye mkojo ingawa ni marachache sana na kwa lugha nyingine inaitwa (hemorrhagic cystitis)

  •  Homa, kutetemeka, mwili kuchoka vinaweza kuwepo kwa mtu mwenye maambukizi kwenye kibofu ingawa vinahusiana na maambukizi ya juu ya mfumo wa mkojo (pyelonephritis)

 

Kumbuka

Historia ya kutoa uchafu ukeni inamaanisha dalili ya maumivu wakati wa kukojoa imesababishwa na  maambukizi kwenye uke, shingo ya kizazi au ugonjwa uitwao pelvic inflamatory disease (PID) ambao hutokea kutokana na maambukizi kwenye mfuko wa uzazi hivo mtaalamu wa afya atachukua historia ya ugonjwa wako ili ajiridhishe kwamba tatizo hili ni UTI na sio jingine. Kwenye historia utaulizwa kama unawapenzi wengi kwa mda uliopita au historia ya kuambukizwa magojwa ya zinaa

Vipimo gani vinafanyika kugundua kwamba una UTI?

Ukifika hospitali baada ya kuchukuliwa historia na kupimwa vipimo vya awali (physical examination) kukagua maeneo husika basi mtaalamu wa afya atachukua vipimo vingine vya maabala kuangalia vimelea kwenye mkojo.

 

Kunavipimo vya haraka visivyo hitaji maabara na kuna kipimo cha damu au wakati mwingine unaweza kuwekewa mpira kwenye njia ya mkojo kwa ajili ya kipimo kwa mtu asiyeweza kukojoa na vingine vingi ikitegemea dakitari anataka kujua nini kinachosababisha ugonjwa huu.

Yapi ni matibabu ya UTI?

Matibabu ya UTI ni ya aina tofauti yakitegemea vipimo na kimelea aliyesababisha ugonjwa huo na ikiwa mwanamke ana ujauzito au la

 

  • Dawa ziitwazo antibiotic hutumika kweye matibabu hayo

  • Kwa mtu aliye na UTI iliyosababishwa na fungasi anaweza kupewa dawa za antifungus

  • Wakati mwingine kama figo haifanyi kazi kwa sababu ya UTI komavu unaweza kutolewa figo hiyo na kuwekewa nyingine kama itawezekana

Yapi mahusiano ya UTI na chakula?
  • Kunywa maji mengi kunasaidia kuondoa wadudu wa UTI kwenye mfumo wa mkojo wakati wa kukojoa

  • Kunywa juisi ya matunda ya cranberry inapunguza kupata UTI kwa kiasi kikubwa kwakuwa hupunguza uwezo wa vimelea vya bakiteria kungangania kwenye kuta za kibofu hivo hutolewa kirahisi wakati wa kukojoa

Vitu vingine unavyoweza kufanya kujikinga/kuzuia UTI ni vipi?
  • Kwa wanawake wanao shiriki tendo la ndoa mara kwa mara na wanaume tofauti wanaweza kukojoa mara baada ya kufanya tendo hilo nahii husaidia kuondoa bakiteria hao wanaoweza kuwa wameingizwa wakati wa kufanya tendo la ndoa

  • Pia kinga ya tahadhari kwa kupatiwa dawa kwa watu wanaopata UTI mara kwa mara inaweza kutolewa

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

12 Septemba 2023, 16:13:28

Rejea za mada hii:

Wein aj, et al., eds. Infections of the urinary tract. In: campbell-walsh urology. 11th ed. Philadelphia, pa.: elsevier; 2016. Https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 17.03.2020

Ferri ff. Urinary tract infection. In: ferri's clinical advisor 2017. Philadelphia, pa.: elsevier; 2017. Https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 17.03.2020

Bladder infection (urinary tract infection—uti) in adults. National institute of diabetes and digestive and kidney diseases. Https://www.niddk.nih.gov/health- information/urologic-diseases/bladder-infection-uti-in-adults. Imechukuliwa 17.03.2020

Urinary tract infections (utis). The american college of obstetricians and gynecologists. Https://www.acog.org/patients/faqs/urinary-tract-infections-utis. Imechukuliwa 17.03.2020

[Guideline] Gupta K, Hooton TM, Naber KG, et al. International clinical practice guidelines for the treatment of acute uncomplicated cystitis and pyelonephritis in women: A 2010 update by the Infectious Diseases Society of America and the European Society for Microbiology and Infectious Diseases. Clin Infect Dis. 2011 Mar. 52(5):e103-20. [Medline]. [Full Text].

[Guideline] Wagenlehner FM, Schmiemann G, Hoyme U, Fünfstück R, Hummers-Pradier E, Kaase M, et al. [National S3 guideline on uncomplicated urinary tract infection: recommendations for treatment and management of uncomplicated community-acquired bacterial urinary tract infections in adult patients]. Urologe A. 2011 Feb. 50(2):153-69. [Medline]. [Full Text].

bottom of page