Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Sospeter M, MD
Dkt. Adolf S, MD
Jumanne, 31 Mei 2022
Madhara ya gono
Gono ni moja ya ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria anayeitwa Neisseria gonorrhoeae. Kimelea huyu mara nyingi huathiri mrija wa mkojo wenye jina la urethra pamoja na shingo ya kizazi kwa wanawake.
Kama gono isipotibiwa kwa wakati au kutobiwa kabisa huweza kusababisha madhara yafuatayo kwa wanawake au wanaume:
Madhara ya gono kwa wanaume
Baadhi ya madhara ya gono iliyoathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume ni:
Makovu kwenye mrija urethra
Kusinyaa kwa mrija wa urethra
Maumivu sugu ya mrija wa urethra
Maumivu ya uume
Utasa
Madhara ya gono kwa wanawake
Baadhi ya madhara ya gono iliyoathiri mfumo wa uzazi wa mwanamke ni:
Makovu kwenye mrija wa falopia
Kusinyaa kwa mrija wa falopia
Maumivu sugu ya tumbo la chini
Utasa
Kusambaa kwa maambukizi kwenye via vingine vya (PID) na nyonga