Mwandishi:
Mhhariri
DKt. Sospeter B, MD
Dkt. Peter A, MD
Jumamosi, 21 Septemba 2024
Mimba nje ya kizazi
Kutungwa kwa mimba nnje ya mfuko wa kizazi hujulikana kitiba kwa jina la ectopic pregnancy au mimba nnje ya kizazi. Aina hii ya mimba hutokea endapo yai lililochavushwa litajipandikiza mbali na eneo maalumu ndani ya kizazi ambapo kwa kawaida yai hujipandikiza.
Mimba hutokea endapo yai limeshachavushwa, kwa kawaida yai lililochavushwa na mbegu za kiume hujipandikiza ndani ya kuta za ndani za mfuko wa kizazi. Mimba nnje ya kizazi mara nyingi hutokea katika sehemu moja ya sehemu ya kizazi, inaweza kuwa kwenye shingo ya kizazi, nje ya utumbo au mrija fallopio. Kwa baadhi ya wanawake mimba hutungwa kwenye/ maeneo karibu na tumbo, utumbo, ovari au shingo ya kizazi.
Mimba iliyotungwa nnje ya kizazi  haiwezi kuendelea kama mimba ya kawaida na endapo yali lililotungishwa litaendelea kuongezeka ukubwa, uharibifu wa mfumo wa kizazi na ogani zingine ndani ya nyonga hutokea na kusababisha damu huvuja ndani ya via vya uzazi.Â
Endapo hali hii itaachwa bila kutibiwa, mama anaweza kupoteza damu nyingi na maisha. Matibabu ya ya mapema husaidia kulinda uzazi dhidi ya uharibifu na kumpa mama nafasi ya kupata mimba nyingine baadaye baada ya afya yake kurejea vema.
Â
Â
Dalili za mimba iliyotungwa nje ya kizazi
Â
Kipimo cha Mkojo
Kama mwanamke akifanya kipimo cha mkojo basi kipimo kitasoma kwamba ana mimba. Hata hivyo mimba hii haitaweza kuendelea kama mimba ya kawaida.
Kutoka damu ukeni na mauivu ya tumbo
Kutokwa damu kidogo ukeni na maumivu ya tumbo au nyonga. Mara nyingi huwa ni dalili za kwanza ya mimba iliyotungwa nje ya mfuko wa kizazi. Kama uvujaji wa damu nyingi kutoka kwenye mrija wa fallopian umetokea, hali hii inaweze kusababisha mwanamke akajisikia maumivu ya bega au  kutaka kwenda haja kikubwa kwa haraka.Â
Â
Dalili hizi hutegemea sehemu damu ilipovilia na mishipa ya fahamu iliyoathirika kwa mvio wa damu hiyo.
Kama mrija wa fallopio umepasuka kutokana na kukua kwa kijusi, damu nyingi itavilia ndani ya tumbo na mwanamke anaweza kupata dalili kama maumivu kiasi ya kichwa, kizunguzungu, kuzirai ama kuzimia.Â
Wakati gani wa kumwona daktari?
Tafuta msaada wa matibabu ya dharura kama utapata dalili zifuatazo zikiwemo zianzoambatana na mimba kutungwa nje ya kizazi;
Maumivu makali ya tumbo au nyonga yakiongozana na kutokwa na damu ukeni
Maumivu ya kichwa yaliyokithiri
KuziraiÂ
Maumivu ya bega
Kuendelea kupata damu baada ya kupata mimba
​
Visababishi vya mimba nnje ya kizazi
Â
Nini husababisha kutungwa kwa mimba nje ya kizazi?
Â
Mimba kutungwa ndani ya mrija wa fallopio huongoza kati ya mimba zilizotungwa nje ya mfuko wa kizazi- mimba hii hutokea endapo yai lililochavushwa limejishikiza kwenye kuta ya mrija wakati linasafili kuelekea katika mfuko wa kizazi na mara nyingi husababiswa na uharibifu katika mirija hii kutokana na mchomokinga (iliyosababishwa na maambukizi kwenye mfumo wa uzazi-PID) au kuwa na umbo la uzazi lisilo la kawaida (tatizo la kuzaliwa au michomokinga na makovu).
Â
Sababu nyingine ni hali ya kutokuwa na kiwango cha kawaida cha vichochezi mwili pamoja na kutofanyika vyema kwa uchavushwaji yai au yai lililochavushwa kutokua kama inavyotakiwa.
​
​
Vitu hatarishi vya kupata mimba nje ya kizazi
Â
Inakadiriwa kuwa mimba 20 katika kila mimba 1,000 zinazotungwa, hutungwa nje ya mfuko wa kizazi. Sababu mbalimbali zinazohusishwa na mimba kutungwa nje ya uzazi ni pamoja na:
Historia ya Mimba  nje ya kizazi .
Kama umeshapata mimba nnje ya kizazi, kuna uwezekano zaidi wa kupata mimba nyingine ya aina hii.
Mchomokinga na makovu au maambukizi.
Â
Kuvimba kwa mirija ya fallopian kutokana na maambukizi au maambukizi ya uzazi, mirija ya fallopian au ovari (ikiwemo michomo kwenye mfuko wa kizazi (pelvic inflammatory disease) huongeza hatari ya mimba kutungwa nje ya uzazi. Mara nyingi, maambukizi hayo husababishwa na ugonjwa wa kisonono au chlamydia.Â
Masuala ya uzazi.
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa kuna mahusiano kati ya matatizo na uzazi - kama vile matumizi ya dawa ya kurudisha uzazi na mimba kutungwa nje ya kizazi.
Maumbile mabaya ya mirija ya uzazi
Mimba kutungwa nje ya uzazi hutokea zaidi kama umbo la mrija wa fallopio limehalibiwa kwa sababu asili au zingine. Umbo hili linaweza kuharibiwa wakati wa upasuaji n.k. Hata kufanyiwa upasuaji kwenye mrija huu wa fallopian unaweza kuongeza hatari ya mimba kutungwa nje ya kizazi.
Uchaguzi wa njia ya Uzazi wa mpango.
Mimba kutungwa wakati wa kutumia kitanzi (IUD) ni nadra sana. Kama mimba ikitokea, uwezekano ni itakuwa nje ya kizazi. Mimba zinazoweza kutungwa baada ya mirija ya uzazi kufungwa, huwa zinatokea nje ya mfuko wa kizazi ingawa ni nadra sana mimba kutungwa baada ya kufungwa kwa mirija ya uzazi yaani fallopio.
Uvutaji wa Sigara
Uvutaji sigara kabla ya kupata mimba tu, huweza kuongeza hatari ya mimba kutungwa nje ya kizazi.​