Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
ULY CLINIC
Jumamosi, 12 Agosti 2023
Ugonjwa wa PID
PID ni ugonjwa unaotokea sana kwa wanawake waliowahi kuathiriwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Asilimia kubwa husababishwa na vimelea vya gonorrhea na chlamydia (wanaosababisha kisonono na pangusa). Ugonjwa huu huweza kubabisha tatizo la kutopata mimba, kati ya wanawake 8 walio ugonjwa huu mwanamke 1 huweza kupata ugumba.
Â
Mara baada ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa na kutotibiwa , vimelea hawa hupanda katika mfulko wa kizazi na hatimaye kufikia katika mirija ya uzazi, wanapokuwa katika mfumo wa kizazi kinga ya mwili huamka kupambana nao. kemikali mbalimbali hutolewa kutokana na mpambano huo na ikiwa ugonjwa umekaa kwa mda mrefu basi kemikali hizi zinazotolewa huharibu kuta za mfuko wa kizazi na kusababisha michomo na mishikamao ya ukuta wa uzazi, mirija ya mayai na viungo vingine vilivyo kwenye uzazi na hivo inasababisha kuwa vigumu kwa mimba kutungwa au kukua katika kuta hizo
Â
Je ni kwa jinsi gani mtu anapata maambukizi haya?
Kwa sababu ugonjwa huu ni matokeo ya kutotibiwa kwa magonjwa ya zinaa(sexually transmitted infection) basi njia zinazomuweka mtu hatarini ni kushiriki tendo la ndoa na mtu aliyeathirika na vimelea hivo. Mambo yafuatayo yanaweza kumweka mwanamke hatarini zaidi
Â
Kupata na kutotibiwa kwa magonjwa ya zinaa
kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
Kuwa na mpenzi mwenye wapenzi wengi
Kuwa na historia ya ugonjwa huu kabla ya sasa
Kujisafisha kwenye kuma kwa maji au vidole
Kutumia uzazi wa mpango hasa kwa kuwekewa vifaa kwenye kizazi
Â
Jinsi gani unaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa huu
Njia pekee ya kuondokana na ugonjwa huu ni kuacha kufanya ngono zembe, ngono kwa njia ya mdomo na mkunduni ni vihatarishi oia vya kupata ugonjwa huu. Endapo umepata mpenzi basi ni vema mkapima na kuangalia kama anamaabukizi ya ugonjwa huu atibiwe kwanza au tumia kondomu unaposhiriki tendo la ndoa.Pia punguza mtandao kwa kuwa na mpenzi mmoja tu mwaminifu aliyepima unaweza kujikinga na ugonjwa huu.
Â
Dalili za PID ni zipi?
Mwanamke anaweza asijitambue kwamba anaugonjwa huu kwa sababu unaweza usiwe na dalili au dalili zinajionesha kidogo sana na hivo kwa kuchukuliwa historia na dakitari pamoja na uchunguzi wa awali (physical examination) na vipimo vingine unaweza kujulikana kama umeathilika na ugonjwa huu. Ikiwa dalili zipo basi unaweza kuwa na dalili kati ya zifuatazo;
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Homa (lakini hutokea kwa mtu mwenye maaambukizi ya awali, ugonjwa ukiwa sugu mgonjwa huwa hapati dalili hii)
Uchafu usio wa kawaida kutoka ukeni na hutoa harufu mbaya
Maumivu au kutokwa damu wakati wa tendo la ndoa
Hisia za kuungua wakati wa kukojoa
Kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi
Â
Je yapo matibabu ya ugonjwa huu?
Ndio yapo matibabu ya ugonjwa huu, matibabu huwa mazuri endapo ugonjwa utatibiwa mapema. Mara utapoanza matibabu dalili zinaweza kutoweka lakini unatakiwa kumaliza dozi uliyopewa. Madhara yaliyosababishwa na ugonjwa huu kwenye kizazi huwa hayaondoki na mtu anapochelewa matibabu madhara yanaendelea kuwa makubwa kama kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai na kuleta makovu katika kizazi
Â
Madhara mengine yatokanayo na ugonjwa huu ni yapi?
Madhara makubwa yatokanayo na ugonjwa huu ni
Kufanyika kwa makovu nnje na ndani ya kizazi yanayosababisha kuziba kwa mirija ya uzazi
Mimba kutunga nnje ya kizaziectopic pregnancy)
Ugumba (infetility)
Maumivu sugu ya tumbo chini ya kitovu /maumivu yasiyoisha