top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatano, 16 Oktoba 2024

Vibarango na Mapunye

Vibarango na Mapunye




Vibarango kichwani ni dalli ya maabukizi kwenye ngozi yanayosababishwa na fangasi Trichophyton na Microsporum ambao husambaa kwenye kope za jicho na  hupenda kudhuru mashina ya vinyweleo. Maambukizi haya hufahamika pia kama Tinea capitis.

 

Ugonjwa huu wa ngozi hutokea sana kwa watoto duniani kote. Unatokea kwa watoto kwa sababu zinazoaminika kwamba  watoto huwa hawana kimelea rafiki aitwaye Pityrosporum orbiculare ambaye huua fangasi hawa. Watu wazima huwa na vimelea hawa na hii ndio maana huaw hawapati maambukizi haya mara kwa mara.

Fangasi hawa huathiri ngozi iliyokua na huweza kusambaa mpaka kwenye ngozi ya kope na sehemu nyingine za mwili.

 

Fangasi hawa pia huambukizwa na husababisha dalili mbalimbali kwenye ngozi.Mara wanapoingia katika ngozi hukua kwa kusambaa kutoka katikati kuelekea pembeni na kutengeneza monekano wa mduara kwa jina jingine kibarango.


Baadaye huvamia sehemu za chini zaidi ya ngozi na mashina ya vinyweleo ndani ya siku ya 12 hadi 14 toka mtu alipoambukizwa na huonekana nje kama miduara ama vibarango kichwani. Vinyweleo vilivyoathiriwa huwa rahisi kukatika na inapofikia wiki ya tatu nywele kukatika huonekana dhahiri.


Ukubwa wa tatizo duniani

 

Ugonjwa huu wa vibarango unatokea kote duniani lakini tatizo linaonekana sana katika bara la Asia na Afrika hasa katika maeneo ya miji. Hari ya maambukizi inaonekana kupungua kutoka asilimia 14 hadi mpaka asilimia 1.2 miaka 50 iliyopita kwa sababu ya kuongezeka kwa usafi wa miji na usafi wa mtu. Huka bara la Ulaya ugonjwa huu hutokea maeneo na maeneo fulani.

Ugonjwa huu hutokea kwa wanaume kuliko wanawake na umri ugonjwa huu unapoonekana sana ni kwa watoto wa miaka 3 hadi 7

 

Dalili za fangasi wa kichwani

 

  • Huanza kama kipele kidogo chekundu(kwa watu weupe) katika kinyweleo maeneo ya kichwani kope za macho na vinyweleo na nyusi

  • Ndani ya siku chache, vipele vidogo vyekundu na mabaka hutokea na nywele hupoteza rangi yake na huvunjika. Mara nyingi huvunjika na kubakisha shina

  • Kasha husambaa, na kutengeneza miviringo na miviringo hii huweza kuungana na miviringo mingine

  • Miwasho huwa kidogo lakini inaweza kuongezeka kwa jinsi muda unavyokwenda 

  • Kukatika kwa nywele maeneo yaliyoambukizwa hutokea pia

Vipimo vya vibarango kichwani

Kuna vipimo aina mbalimbali vinavyoweza kufanyika, nywele au magamba kutoka katika sehemu iliyoathiriwa huchukuliwa na kwenda kupimwa kwa kemikali au kungaliwa kwa darubini.


Matibabu ya vibarango kichwani

 

Matibabu yapo ya aina mbalimbali

 

Uchaguzi wa matibabu ya vibarango hutegemea aina ya fangasi aliyeathiri vinyweleo, kusambaa kwa fangasi na wakati mwingine hali ya afya ama kinga ya mwili ya mgonjwa.

  • Kutumika kwa dawa ya kunywa ya aina ya griseofulvin hutoa matokeo mazuri sana

  • Pia dawa za kupaka wakati mwingi huwa hazileti matokeo mazuri kwa jinsi inavyotakiwa na mgonjwa anaweza asipone fangasi

  • Dawa mpya za fangasi kama itraconazole, terbinafine, na fluconazole, zimelipotiwa kutoa matokeo mazuri kama dawa mbadala dhidi ya fangasi hawa wa kichwanikati ya dawa zote hizo dawa hizi mbili, itraconazole na terbinafine hutumika sana

  • Selenium sulfide shampoo huwezakuzuia kusambaa kwa ugonjwa na kupunguza vimelea pia

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

16 Oktoba 2024 06:36:44

Rejea za mada hii:

Alopecia, ABCs of Dermatology toleo la 4, 2003

Kliegman RM, et al. Cutaneous fungal infections. In: Nelson Textbook of Pediatrics. 20th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2016. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 10.03.2020

Treat JR. Tinea capitis. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.11.2020

Kaushik N, et al. Superficial fungal infections. Primary Care Clinics in Office Practice. 2015;42:501.

Ringworm risk and prevention. Centers for Disease Control. http://www.cdc.gov/fungal/diseases/ringworm/risk-prevention.html. Imechukuliwa 10.11.2020

Allmon A, et al. Common skin rashes in children. American Family Physician. 2015;92:211. Bennett JE, et al. Dermatophytosis (ringworm) and other superficial mycoses. In: Mandell, Douglas, and Bennett's Principles and Practice of Infectious Diseases. 8th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2015. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 10.11.2020

bottom of page