Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Jumatano, 16 Oktoba 2024
Vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo ni vidonda vinavyotokea ndani ya kuta za tumbo na huhushisha umio yaani mrija unaoingiza chakula kwenye tumbo, tumbo ama na Duodenamu ambapo ni sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba mara baada ya tumbo.
Â
Hivo vidonda vya tumbo huweza kugawanya katika aina tatu
Â
1.vidonda ndani ya mrija unaopeleka chakula kwenye tumbo (esophagus)
2.vidonda vya tumbo ndani ya tumbo(gastric) Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â
3. Na vidonda vya tumbo kwenye mrij unaotoa chakula katika tumbo ama (duodenum)
Â
Kwa sasa madaktari wanajua kwamba maambukizi ya bakiteria au baadhi ya madawa yanaweza kusababisha vidonda vya tumbokwa asilimia kubwa zaidi ukilinganisha na chakula na ama msongo wa mawazo
Â
Dalili za vidonda vya tumbo
​
Maumivu ya tumbo huwa ni dalili kuu, maumivu haya huwa ya aina ya kuunguza. Maumivu hayo hutokana na vidonda haswa pale tindikali iliyopo tumboni inapokutana na vidonda hivo na kuviunguza zaidi
​
Maumivu hayo yanaweza;
Kutokea sehemu yoyote kati ya kitovu na sehemu ya kifua karibu na chuchu
Kuongezeka ukila chakula
Kupungua ukila chakula
Kuongezeka wakati wa usiku
Kupungua kwa muda unapokula vyakula ama vinavyopunguza makali ya tindikali tumboni ama unapotumia dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni
Kupotea na kutokea baada ya siku/wiki chache baadae
                         Â
Dalili zingine za vidonda vya tumbo ni kama vile
​
Kwa mara chache sana vidonda vya tumbo vinaweza kusababisha dalili kali sana kama vile
Kutapika damu-nyekundu ama nyeusi
Kinyesi kuwa cheusi kinaweza kuwa cheusi kama rami pia
Kichefuchefu na Kutapika
Kupoteza uzito bila sababu
Kubadilika kwa hamu ya kula
Vidonda vya tumbo
​
Vidonda vya tumbo ni vidonda vinavyotokea ndani ya kuta za utumbo kuanzia kwenye mpira unaoingiza chakula kwenye tumbo, tumbo ama na sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba mara baada ya tumbo. Hivo vidonda vya tumbo huweza kugawanya katika aina tatu
​
1.vidonda ndani ya mrija unaopeleka chakula kwenye tumbo (esophagus)
2.vidonda vya tumbo ndani ya tumbo(gastric) Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â
3. Na vidonda vya tumbo kwenye mrij unaotoa chakula katika tumbo ama (duodenum)
Â
Nini husababisha vidonda vya tumbo?
Â
Vidonda vya tumbo hutokea endapo tindikali ndani ya utumbo zitapenyeza na kula ukuta wa ndani wa tumbo na kuleta vidonda katika maeneo kabla ya tumbo tumboni na baada ya tumbo. Mfumo wa tumbo umefunikwa kwa juu na ukuta wa uteute kama mlenda ambao huzuia tindikali hizi kupenyeza na kula nyama za kuta za tumbo. Hivo kama uteute huu ukipungua ama kama uzalishaji wa tindikali ukiongezeka basi mtu anaweza kupata vidonda vya tumbo. Sababu kuu zinazoweza kusababisha ni;
Maambukizi ya bakiteia aina ya H pylori. Bakteria huyu huishi katika uteute ambao hufunika kuta za juu za tumbo dhidi ya muunguzo wa tindikali. Bakiteri ahuyu huwa na tabia ya kuzalisha baadhi ya vimiminika ambavyo huharibu uteute huu na kusbabisha kuunguzwa kwa ukuta wa juu wa tumbo na kuleta vidonda vya tumbo. Pia bacteria huyu huweza kuzunguka katika uteute na kusababisha mashimo ambayo tindikali hupita na kuunguza ukuta wa tumbo
Chakula na dawa- Baadhi ya vyakula na dawa huweza kusababisha vidonda vya tumbo endapo zitatumiwa kwa mda mrefu, dawa hizi ni zile za kuondoa maumivu na ni jamii aina ya (NSAID)aspirini, kama aspirini, diclofenac,ibuproren, naproxen ketoprofen na zingine jamii hii
Vidonda vya tumbo hutokea sana kwa wazee wanaokunywa dawa hizo kwa sababu ya kuondoa maumivu ya viumgo vya mwili ama wanaotumia kwa ajili ya tatizo la osteoarthritis.
Dawa zingine zinazotibu osteoarthritis yanayoweza kusababisha vidonda vya tumbo ni kama vile biphosphonate na virutubisho vya potassium
​
Kurithi uzalishaji tindikali wa kiwango cha juu. Kuna baadhi ya watu wanatatizo la uzalishaji wa tindikali kwa wiki katika kuta za tumbo , hali hii inasababisha kuungua kwa kuta za tumbo na kupelekea tatizo la vidonda vya tumbo
Kuwa na Saratani katika chembe zinazozalisha tindikali tumboni.
​
Vihatarishi vya kupata vidonda vya tumbo
Â
Uvutaji wa sigara
Unywaji wa pombe--huchoma na kusababisha vidonda katika tumbo na pia huongeza uzalishaji wa tindikali
Madhara ya vidonda vya tumbo
Huweza kupelekea
Kutoboka kwa kuta za tumbo-kusababisha maumivu makali sana ya tumbo ambayo hujawahi yasikia
Kuvuja kwa damu ndani ya tumbo
Maambukizi ndani ya ukuta unaofunika matumbo
Makovu ndani ya tumbo
​
Vipimo na matibabu
 Yapo matibabu ya aina tofauti, hutegemea ni nini kinachosababisha tatizo hili kutokana na vipimo vilivyofanyiaka
Vipimo vinavyoweza kufanyika ni kama vile
Kipimo cha kutambua uwepo wa bakiteria wa H pylori kwenye damu, kinyesi ama kipimo cha kutambua gesi aina ya urea kwenye pumzi ambayo hutole na bakiteria huyu.
Kipimo cha kutumia kamera inayoonyesha mfumo wa tumbo ama endoscope- ni kizuri kwani huonesha kidonda kilipo na kuchukua kinyama kwa ajiri ya uchunguziKipimo cha Xray endapo unadalili za kutoboka kwa ukuta wa tumboÂ
Dawa zinazotumika
​
Dawa za kutibu maambukizi ya bakiteria wa Hpylori
Dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali
Dawa za kusiamisha uzalishaji wa tindikali
Dawa zinazopunguza makali ya tindikali iliyozalishwa
Dawa zinazoongeza uteute katika kuta za tumbo