Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 28 Oktoba 2021
Vipele vya UKIMWI
Vipele ni moja ya dalili ya magonjwa ya ngozi yanayotokea sana kwa watu waishio na VVU au UKIMWI na huweza kuwa ishara ya kwanza ya maambukizi ya VVU.
Asilimia karibia 90 ya watu wenye maambukizi ya VVU hupata magonjwa ya ngozi na wengi huugua zaidi ya ugonjwa mmoja wa ngozi.
Magonjwa ya ngozi yanayoongoza kutokea ni fangasi, ikifuatiwa na izima na demataitis ya seboreiki.
Magonjwa ya ngozi yaliyozungumziwa katika makala hii ni yale yanayosababisha vipele kwenye ngozi ya waishio na VVU ambayo ni;
Uvimbe wa tezi limfu
Hutokea kama sehemu ya sindromu ya maambukizi makali ya VVU. Asilimia 70 ya wagonjwa hupatwa na dalili na ishara za;
Homa
Vidonda kooni
Kuvimba mitoki ya shingo
Kutokea kwa harara au vipele vidogodogo mwilini
Vipele na harara huonekana kama vipele vidogo na mabaka mekundu kwa watu wenye rangi nyeupe na hutokea sana sehemu kubwa ya mwili na wakati mwingine huweza tokea kwenye viganja vya mikono, chini ya kanyagio, maeneo ya siri na mdomoni pia.
Penisiliosis
Hutokana na uambukizo wa fangasi Penicilllium marneffei. Vipele hivi hutokea kwa nadra.
Sifa za vipele vya penisiliosis
Hutoa ishara za;
Vipele vidogo vyenye mwonekano wa kitovu
Kidonda
Upele mkubwa
Upele unaoambatana na mabaka
Upele mithiri ya chunusi
Folikulaitis
Basilari angiomatosis
Basilari angiomatosis ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya Bartonella henselae na Bartonella quintana.
Maambukizi haya huweza tokea kwenye ogani ndani ya mwili au kwenye ngozi na huwa na mwonekano wa uvimbe kwenye kwenye ngozi wenye jina la angioma unaotokana na kuzalishwa kwa mishipa mipya ya damu na kukua kwa sehemu ya kuta zake pasipo dhibiti.
Hutokea sana kwa wagonjwa wenye CD4 chini ya 100 na wenye historia ya ya kukwanguliwa au kung’atwa na paka. Ugonjwa huu wa ngozi hutokea kwa nadra.
Sifa za upele/uvimbe
Sifa za vipele vya Basilari angiomatosis ni
Huweza kutokea mmoja au kwenye makundi
Huwa na rangi nyekundu au zambarau
Huweza tokea kwenye kope za macho, ngozi laini, ini na bandama
Huweza tibiwa na dawa erythromycin, doxycline au minocycline.
Vipele vya TB
Ugonjwa wa TB au ugonjwa wa Mycobacteria husababishwa sana na bakteria Mycobacterium tuberculosis, Mycobacterium avium intracellulare (MAI), na mara chache sana Mycobacterium kansaii, Mycobacterium fortuitum na wengine. Ugonjwa huu ni nadra kutokea.
Sifa za vipele
Vvipele vya TB kwa mgonjwa wa VVU ni;
Huweza kuwa na mwonekano wa vipele vidogo
Huweza kuwa kama nundu
Huweza kuwa gamba jekundu maeneo ya magoti, mgongo wa chini na kiwiko cha mkono na huweza washa au kuuma.
Huweza kuwa kama upele mkubwa wenye usaha ndani yake
Huweza kutengeneza mwonekano wa jipu
Vipele vya kirusi herpes simplex (HSV)
Maambukizi ya kirusi hutokea sana kwa wagonjwa wanaoishi na VVU na kutokea kwa wagonjwa hawa humaanisha mara nyingi kuamshwa kwa virusi vilivyolala.
Sifa za vipele
Ugonjwa huu hutengeneza vipele vyenye sifa zifuatazo;
Malenge madogo yaliyo kwenye mkusanyiko maeneo ya ndani ya midomo na kwenye ngozi laini ya maeneo ya siri
Vipele vya folikulaitis usoni
Vidonda vidogo au vyenye kina kirefu
Vipele vya kirusi Varicella zoster (VZV)
Maambukizo ya VZV huweza tokea kwenye hatua yoyote ya UKIMWI. Dalili na ishara za ugonjwa huwa hazina tofauti kwa mgonjwa mwenye VVU au asiye na VVU.
Sifa za vipele
Mara nyingi hufanana na vipele vya HSV
Huweza zalisha vipele vyenye sifa tofauti mfano vipele vinavyofanana na vinundu vyenye kidonda kwa juu.
Molluscum contagiosum
Husababishwa na kirusi pox ambacho huathiri chembe za ngozi zenye jina la epidermal.
Sifa za vipele
Vipele vya Molluscum contagiosum huwa na sifa zifuatazo;
Hutengeneza mwonekano wa vipele vidogo vyenye kitovu katikati maeneo ya siri na usoni.
Huweza tengeneza pia upele mkubwa kwa wagonjwa wenye maambukizi sugu ya UKIMWI
Human papillomavirus (HPV)
Husababisha vipele vyenye jina la verruca vulgaris na condylomata acuminate au kwa jina vyenye mwonekano kama sunzua au uyoga uliosambaa. Huweza tokea maeneo ya ngozi laini kama ukeni, kwenye uume, mdomoni, usoni na kwenye njia ya haja kubwa.
Sifa za vipele
Huongezeka kwa jinsi kiwango cha CD4 kinvyopungua kwenye damu.
Mwonekano mwingine e ni kama vinavyoonekana kwenye picha inayofuata;
Cutaneous cytomegalovirus (CMV)
Ugonjwa uliosambaa hutokea sana kwa wagonjwa waishia na maambukizi ya VVU hata hivyo huweza tokea pia kwenye ngozi.
Sifa za ugonjwa wa CMV kwenye ngozi
Kuzuka kwa vipele vidogo vyenye maji
Kutokewa na vipele vidogo visivyo na maji
Kutokewa na vinundu vikubwa au verishas
Kaposi's sarcoma
Ni saratani ulayoathiri chembe za ukuta wa ndani wa mishipa ya damu na huweza kusababisha dalili za vipele vyenye rangi ya zambarau kwa watu weupe na dalili zingine kutokana na eneo lililoathiriwa.
Sifa za vipele
Saratani ya kaposis mara nyingi husababisha ngozi kupata madoa yenye rangi ya zambarau, pinki, kahawia, mweusi, bluu au mwekundu na wakati mwingie hutengeneza upele wenye sifa zifuatazo.
Hutengeneza mwinuko kiasi kwenye ngozi unaostahili kuitwa upele
Huweza tengeneza mwinuko mkubwa unaostahili kuitwa nundu
Upele wake hauna maumivu
Huwa na rangi ya zambarau, pinki, kahawia, mweusi, bluu au mwekundu ikitegemea rangi ya ngozi yako
Unaotokea sana maeneo ya paja, miguu, kanyagio na uso
Upele unaweza tokea pia kwa nadra maeneo ya macho, koo na mengine ndani au nje ya mwili
Vipele vinavyoambatana na VVU
Ilifahamika mwanzoni kuwa, vipele ni ishara ya maambukizi ya UKIMWI na hivyo kusema kuwa vipele vinavyotokea kwa wagonjwa wa UKIMWI huitwa kwa jina la vipele vinavyoambatana na VVU au PPE. Vipele vya PPE huashiria aina kadhaa ya vipele ambavyo vimeorodheshwa hapa chini.
Vipele vya folikulaitis ya ki-esinofilia
Ni aina ya vipele vya PPE vinavyotokea sana na huathiri watu wenye maambukizi ya VVU.
Sifa za vipele
Huwasha sana
Hutokana na kuvimba kwa shina la nywele
Huwa na rangi nyekundu
Vipele huweza kuwa na usaha au bila usaha
Hutokea kwenye kiwiliwili na kwa nadra usoni na shingoni.
Maambukizi ya foliko
Vipele hivi hutokea pale shina la nywele linapopata maambukizi ya bakteria, kimelea Demodex Folliculorum na fangasi mwenye jina la Malassezia.
Vipele hivi huwasha huwa na mwonekano wa vipele vilivyotajwa hapo juu.