top of page

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

​

Magonjwa ya aleji ya atopic hutokwa kwa kuambatana na kupiga chafya sana, kutokwa na mafua, na ngozi kupata vipele vidogo


 

Magonjwa ya atopic uhusisha, pumu yangozi, kutokwa na mafua na macho kuuma pamoja na pumu ya ngozi yameongezeka sana katika karne ya 19.

Magonjwa haya yanaweza kuwa yanasababishwana mazingira au kurithi vinasaba vinavyosababisha tatizo hili.


 

Sababu za kimazingira

Mazingira ni kiamuzi kikuu cha kuonekana kwa tatizo la atopic, ushahidi mkuu unaonyeshwa kwa utofauti wa ugonjwa huu mkoa na mkoa, kwamba baadhi ya mikoa ugonjwa upo kwa kiwango kikubwa zaidi ya mikoa mingine


 

Sababu za kijeni

Magonjwa ya atopic huwa na uhusiano mkubwa na sababu za kurithi za kijeni, endapo wazazi wote wawili wameathirika na tatizo la atopic, au ndugu na jamaa, kwa asilimia 40% ya watoto atakaowazaa watapatatatizo la atopic. Inasemekana kwamba watoto wenye geni za kusababisha tatizo la atopic wana uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la aleji na vitu vingine sana.


 

  • Utambuzi wa ugonjwa

  • Magonjwa ya atopic hutokea na dalili zifuatazo

  • Huanza kuonekana uchangani

  • Asilimia 40 ya watoto wenye tatizo hili watapata asthma aukutokwa na mafua pamoja na macho kuuma na dalili za kuumwa kifua kabla ya kufikia umri wa miaka mi 5.

  • Pumu ya ngozi- miwasho ya ngozi, huonekana kama harara au vipele vidogo vinavyojirudia rudia, dalili muhimu ambata ni ngozi kukauka, ngozi kuwa ngumu na historia ya tatizo la atopic, keratosisi na kuwa na mishipa isiyo ya kwaida kwenye ngozi katika familia.

  • Pumu ya kifua-Dalili zinahusisha kuziba kwa njia za hewa ndani ya kifua, kutoa miruzi kunakiamshwa na mambo kama mazoezi, maambukizi ya virusi, aleji/mzio). Dalili hizi huondoka endapo mgonjwa amepata dawa za kuzibua njia za hewa.

  • Tatizo la kutokwa mafua na macho kuwasha- kutokwa mafua, kupiga chafya na kuwashwa pua na macho ni dalili zinazotokea sana. Dalili hutokea kwa msimu Fulani na husababishwa na mzio.

​

Vipimo

​

Kipimo cha kutambua endapo mtu ana mzio na vitu katika mazingira hufanyika kwa kupima uwepo wa protini kwenye damu inayoitwa IGE ambayo huwepo kwenye damu kwa mtu huyu. Mgonjwa ambaye anatakiwa kupima kipimo hiki ni

Endapo mtu ana pumu ya ngozi kipimo kitafanyika endapo mgonjwa anapata dalili kwa vumbi la ndani ya nyumba au anapata mzio na vyakula anavyokula

Kama anapumu ya ngozi- kipimo hufanyika endapo kuna umuhimu wa kutambua tatizo la pumu ya ngozi


 

Na kama ana tokwa mafua na macho kuwashwa basi kipimo kitafanyika endapo anapata dalili kwa vumbi ndani ya nyumba, au endapo kufanya hivyo kunatakiwa kufanya utambuzi wa tatizo hili au endapo dawa ya kupambana na kinga ya mwili zinatakiwa kutumika.


 

Matibabu

Mpaka sasa hakuna matibabu ya kutibu mzio, matibabu yaliyopo sasa ni kupambana na dalili zinazotokea au kuepuka visababishi vya mzio. Matibabu yanaweza kuwa ya dawa za kupambana na dalili au za kushusha kinga za mwili zisiamke endapo mtu atakuwa kwenye mazingira yenye vitu ambavyo vinamsababishia mzio.


 

Kusoma zaidi kuhusu makala hizi au kwa maswali Piga namba zilizo chini ya mtandao huu.

​

​

Toleo la 2

Limeboreshwa 5/12/2018

bottom of page