top of page

Majibu ya maswali mbalimbali

Je, mimba huonekana kwenye kipimo cha mimba kuanzia siku ngapi?

Kipimo cha mkojo hugundua homini ya ujauzito siku 7-14 baada ya uovuleshaji, huku kipimo cha damu hugundua mapema zaidi yani siku 6-8. Vipimo vya ultrosound huchelewa kugundua uwepo wa mimba.

Kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi

Kutokwa na damu kati ya hedhi husababishwa na mabadiliko ya homoni, magonjwa ya via vya uzazi, maambukizi, au saratani. Matibabu hutegemea chanzo na yanaweza kujumuisha dawa za homoni, antibiotiki, au upasuaji.

Ni yapi madhara ya Misoprostol?

Misoprostol husababisha maumivu ya tumbo, kutokwa na damu, kichefuchefu, na kuhara, lakini pia inaweza kusababisha madhara makali kama kutokwa na damu nyingi au maambukizi. Ikiwa una dalili kali, unapaswa kutafuta msaada wa kitabibu haraka

Doxycycline inatibu nini?

Doxycycline inatibu nini?

Ni antibiyotiki inayotoka kwenye kundi la tetracyclines na hutumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria mbalimbali. Pia ina matumizi mengine yasiyo rasmi, kama vile kuzuia malaria na kutibu chunusi.

Unasisimuaje G spoti?

Mtu anaweza kutumia kidole (haswa kidole cha shahada) kwa kukipinda kwa namna ya ishara ya "njoo" kuelekea kwenye ukuta wa juu ya uke. Kupapasa taratibu eneo hili kunaweza kusababisha hisia za kufurahia au hamu ya kukojoa.

G spoti ni nini?

Ni sehemu ndani ya uke wa mwanamke inayodhaniwa kuwa na msisimko mkubwa wa kingono ikisisimuliwa.

Unaweza kupata mimba baada ya kutoa Mimba?

Je, unaweza kupata mimba baada ya kutoa mimba?

Mzunguko wa hedhi

Mzunguko wa hedhi ukoje?

Mzunguko wa hedhi huanza kuhesabiwa siku ya kwanza kuona hedhi moja hadi siku ya kwanza ya kuona hedhi inayofuata, kwa kawaida huchukua siku 21 hadi 35. Mzunguko huu kwa wanawake wengi huanza katika umri wa miaka 12.

Ni muda gani sahihi wa kushiriki ngono baada ya mimba kutoka?

Unaweza kuanza kushiri ngono baada ya mimba kutoka mara tu unapokuwa tayari. Lakini kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza kushiriki.

Je, unaweza kujifungua kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji katika ujauzito uliopita?

Unaweza kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji endapo sababu ya upasuaji haijirudii na mwenendo wa leba ni mzuri.

Ni zipi dalili za mtoto kushuka kwa ajili ya kutoka (kuzaliwa)?

Kushuka kwa mtoto katika nyonga ya uzazi huanza kutokea katika wiki za mwisho za ujauzito, hatua hii ni muhimu sana kwani humuuandaa mtoto na mama kuingia hatua ya leba.
Mama mjamzito anapswa kutambua dalili na viashiria mbali mbali vya kushuka kwa mtoto.

Dawa zenye muingiliano na maziwa

Baadhi ya dawa zikitumika pamoja na maziwa au mazao ya maziwa husababisha muingiliano, hivyo kupunguza ufanisi wa dawa.
Unashauriwa kunywa maziwa masaa machache kabla au baada ya kunywa dawa ili kuzuia muingiliano.

bottom of page